
Mheshimiwa Balozi ย Mbundi, tareheย 15 Januari, 2021, aliongoza majadiliano baina ya Poland na Tanzania.
Mjadiliano hayo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano hususan katika masuala ya biashara na ย uwekezaji. Kwa upande wa Tanzania washiriki walikuwa ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo; Mjumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango; Watendaji wa NFRA; na Watendaji wa TBA.Kwa upande wa Poland, walioshiriki ni pamoja na ย Mheshimiwa Krzysztof Buzalski Balozi wa Poland nchini Tanzania na Wawakilishi wa makampuni kutoka Poland ya Feerum S.A na Unia Spzo.o.








