0 0
Read Time:2 Minute, 0 Second

Na Dr Yahya Msangi

Mama kwa utaratibu uliopo haya yanawezekana:

-NAFASI YA SPIKA INAWEZA KUHODHIWA NA MTU AU KIKUNDI KWA MASLAHI YAKE AU YAO.

-TUNAWEZA KUCHAGULIWA SPIKA NA MATAIFA AU MAKAMPUNI AU MATAPELI WA KIMATAIFA.

  • MTU ASIYE NA UWEZO ANAWEZA KUWA SPIKA.

Nafasi ya spika ni kubwa mno kwenye taifa lolote. Ni sawa na ya wakuu wa mihimili mingine kwa ustawi was taifa. Haifai kufanyia mzaha uchaguzi wa Spika.

Tunaweza kufanya yafuatayo:

  1. Kila chama kichuje wagombea uspika kwa kutumia vikao vya chama husika. Mfano mwanachama anayetaka uspika awasilishe Omni lake katika kikao cha juu cha maamuzi cha chama chake. Anayeteuliwa na kikao cha chama ndio jina liwasilishwe bungeni na chama chake. Tusiache wabunge wa chama ndio waamue nani awe mgombea uspika kutoka miongoni mwao. Kuna mgongano mkubwa wa maslahi. Spika sio kiongozi wa wabunge was chama peke yao. Ni kiongozi wa bunge ambalo raia wote linatuhusu. Kwa utaratibu wetu Spika ndiye msimamizi wa maslahi na mapato ya wabunge. Anaweza kutumia madaraka haya kupata uspika kama ambavyo tumeona spika wa sasa wakati akiomba kura akiwaaahidi wabunge maboresho ya “yale mambo yetu”!
  2. Tunaweza kuruhusu uspika ugombewe na hata asiye mbunge. Hata Marekani sio lazima Spika wa Congress awe mjumbe wa Congress au Senate. Mara kadhaa uspika umegombewa na watu nje ya congress japo mara zote wameshindwa kwa kuwa wapiga kura huwapigia wa vyama vyao.
  3. Nafasi ya uspika inaweza kutangazwa watu waombe. Pawe na jopo la kupitia sifa za waombaji na kuwahoji. Wahojiwe hata na wananchi kupitia TV. Spika aajiriwe kama ambavyo Katibu wa Bunge anaajiriwa. Akiharibu afukuzwe kama mtumishi yoyote. Mfano spika akiacha kusimamia majadiliano ya bajeti akajikita kujadili ujenzi was mradi wenye kuhujumu nchi itakuwa rahisi kumfukuza asiharibu nchi. Aondoke akafanye udalali akiwa nje ya chombo cha kutunga sheria. Asitumie uspika kufanya udalali. Ikiwa Jaji Mkuu hatuwaachii majaji wamteuewe kwa ni kwa spika tuache wabunge wamteue? Kuna ajabu gani kumuajiri spika sawa na Jaji Mkuu?
  4. Msimamizi wa uchaguzi wa spika awe mtu asiye mbunge au mtumishi wa bunge. Afrika Kusini msimamizi sa uchaguzi wa Spika ni Jaji Mkuu (Chief Justice). Haifai kuacha wenye maslahi msigano (conflict of interest) ndie asimamie uchaguzi was Spika kama tufanyavyo.

Nîmalize kwa kukumbusha kuwa utaratibu uliopo sa kumpata Spika uliwekwa kwenye katiba na Sheria zetu na mtu ambaye baadae alikuja kuwa spika! Ina maana alijiwekea mazingira mazuri. Askari umefika sasa kubadili. Hâta chama tawala nadhani Sasa wameona ubaya wa utaratibu uliopo!

Ngoja nifuturu! Alamsiki!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %