0 0
Read Time:4 Minute, 1 Second

Na Dr Yahya Msangi

Yanayojiri kwa jirani zetu Tchad (Djamena ni mwendo wa saa 12 kwa bus kutoka Lomé) yamefanya nikumbuke matukio kadhaa yaliyonikuta maishani. Moja likihusu wasenegali na mlima Kilimanjaro, lingine waithiopia na bahari. Lakini leo niongelee tukio moja nililokutana nalo enzi za NAFCO (wasangu n’a wabena n’a wanyakyusa wakiita NAFUU HUKO). Mwaka 1992 nilipokuwa Meneja Uzalishaji (Production Manager) pale NAFCO KAPUNGA tulitembelewa na ujumbe toka Saudia ukiambatana na wajumbe toka Baraza la wawakilishi Zanzibar. Walikuja kutembelea shamba na kuona ni jinsi gani Saudi Arabia wataweza kununua mchele.Walikuja kipindi tunavuna mpunga. Kipindi kile baada ya mpunga kuvunwa ulikuwa unapelekwa kumwaga kiwanjani karibu na mashine ya kukobolea. Hii ilikuwa ndio mashine ya kisasa kuliko site Africa. Kutokana na ukubwa wa shamba mpunga ulikuwa ubamwagwa kiasi unakuwa kama mlima ukiutizama kwa mbali. Sasa wakati nawapeleka kiwanjani wakaone mpunga mwarabu mmoja akaniuliza “kumbe na nyie mna mchanga kama sisi?” Nikamuuliza umeona mchanga? Akanijibu “si ule kule mbele? Nilicheka sana! Nikamwambia ule ni mpunga sio mchanga! Mwakilishi mmoja toka Zanzibar akamaka “toba, ule mlima ni mpunga”? Sasa tulipofika kwenye “mlima” wale waarabu wakauliza “mbona huu sio mchele”? Kumbe hawajui mchele unapatikanaje! Nikawaingiza kwenye kinu wakaona mpunga unavyokobolewa kutoa mchele! Walistaajabu sana! Kiongozi wao akaniambia sisi tukijua mchele unapatikana shambani! Yaani wait wakijua kinachovunwa shambani ni mchele qui mpunga! Tulicheka sana! Tukio hili na hayo mengine yalinipa funzo kuwa kuna mambo au hali au vitu hatuvitilii maanani kwa kuwa tu tumevizoea!Tanzania kuna vitu tumevizoea mno mpaka hatuvithamini. Nivitaje vichache:1. Kubadilishana uongoziTanzania tuna utaratibu Bora mno hâta kushinda baadhi ya nchi zilizoendelea. Chukulia kinachojiri Tchad hivi sasa. Katiba inataka spika wa bunge (na katiba zote za makoloni ya mfaransa zinataka hivyo) ndiye awe mkuu wa nchi pindi raisi atakapokufa au kuachia madaraka kwa sababu yoyote île. Spika wa bunge la Tchad kakataa kushika ugaidi kama katiba inavyoelekeza! Badala yake karidhia mtoto wa marehemu atwae ikulu! Tabia hii ya Spika kukataa Kiti sio mara ya kwanza kutokea kwenye makoloni ya mfaransa. Popote pale ambapo mtoto wa raisi alichukia kiti cha babaake ujue Spika alikataa! Katoka nchi mmoja Spika aliondoka zake kwenda likizo Paris akiacha ombwe lililopelekea mtoto wa raisi kuchukua kiti kwa madai Spika kakimbia! Ilikuja bainika Spika aliwezeshwa na mtoto wa Marehemu aende zake kula bata Paris! Huwa najiuliza n’a sie katiba ingetaka Spika ashike kiti ingekuwaje? Mhhhh! Bora waliotunga katiba waliona mbali! Tanzania tuenzi utaratibu wetu! Ni mzuri. Wapo wanaoubeza lakini hawa ndio wale wamekalia dhahabu lakini hawajui!2. Uongozi huruUkitizama Tchad n’a makoloni mengine ya mfaransa tatizo ni uongozi kuwa vibaraka wa mkoloni. Hawachaguliwi na wananchi bali na mkoloni. Wananchi wanapoteza muda kupiga kura! Ikiwa mkoloni hakutaki huchaguliwi na ukichaguliwa utaondoka tu! Sankara na Bagbo ni mifano hai. Mfaransa kama hakutaki ama upinduliwe, uuze au ushitakiwe kwa uhalifu. Hussein Habré kafungwa kwa mahakama ya hovyo aliyounda mfaransa nchini Sénégal. Habré akitukana na kudhalilishwa ndani ya mahakama. Hukumu ilijulikana hâta kesi haijaisha! Kwa miaka kadhaa sasa raia nchi mbalimbali ikiwemo Tchad wakiendesha kampeni ya kujitapa shirikisho la faranga kwa kuchoma moto noti hadharani ! Mfaransa hataki! Anadai wakati wa majadiliano ya kuwapa uhuru walikubaliana yéyé ndio atasimamia hela! Bora Kagame alisepa aisée! Wizi mtupu!Tanzania hatujawahi kumpata kiongozi sampuli hiii. Watakuwa na mapungufu kama binadamu yoyote lakini kwamba wamepachikwa ikulu na Mwigereza hapana! Cha ajabu kuna wenzetu siku hizi wanapinga viongozi wetu kulinda raslimali dhidi ya wakoloni! Wanaona fahari kutumika na wakoloni kuhujumu nchi yao! Na makazi wamehamishia huko! Hawa nao wamekalia dhahabu lakini hawana habari! 3. Kutokuwepo udini na ukabilaKatika makoloni ya mfaransa mara tu ukifika n’a kuishi hutasita kuona ukabila n’a udini wa wazi. Mifano ni mgawanyo wa maeneo ya kuishi mijini. Utaona waislam wanaishi eneo linaitwa “zongo” au “madina” Ukisikia eneo linaitwa zongo au Madina ujue kama wee mkristo utapata shida kuishi haoo. Vivo hivyo kwa wakristo. Hawana jina maalum la maeneo Ila kama wee mwislamu utahisi hapa sitakiwi! Na hiki ndio kiliharibu Afrika ya Kati. Ilitoka hoja bungeni ikaungwa mkono na Spika kuwa waislam wote waondoshwe mji mkuu! Wakaondoshwa na misikiti ikavunjwa! Waislam wakawaita Tourag kuwasaidia! Kikawa kivumbi hadi kesho! Ni hivyo hivyo burkina faso! Ukienda Cameroun nchi imegawanyika kikabila na kilugha! Tanzania udini na ukabila umedhibitiwa sana. Tanzania makabila yanataniana! Huku kwa wenzetu makabila hayataniani! Ukitania Kabila jingine unaweza kusababisha balaa! Tanzania raisi Mkristo anavaa kanzu na barghashia. Tanzania kiongozi mwislamu anaingia kanisani. Kwa wenzetu anaweza kuuawa au kukosa kura! Bahati mbaya siku hizi wapo wenzetu haswa wa udini wanataka kutuletea udini wao nchini. Wamejigeuza wanasiasa wa upinzani. Hawahubiri tena neno! Wao wakipanda madhabahuni ni katiba, tume, hali ya maandamano! Hawa nao wamekalia dhahabu hawajui! Kwa leo niishie hapa Nadhani ujumbe umefika? Nihitimishe kwa kusema Tanzania ina mazuri mengi lakini tusipoyalinda tunaweza kuwa kama kina Tchad !Onyo: kama wee akili ya wale bungeni wanaojivunia darasa la 7 pita zako. Na waambie wanao “someni mpaka la 7 halafu rudini tulime”😊😊😊😊😊😊

LoméTOGO

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %