0 0
Read Time:49 Second

Mkoa wa Pwani

Tarehe 15 Julai 2021, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Eng. Mwanasha Tumbo alifanya ziara kwenye viwanda vya kusindika matunda vya Sayona Fruits Ltd kilichopo Mboga Chalinze na Elven Agri kilichopo Mapinga Bagamoyo. Habari picha hizo ni baadhi ya matukio kwenye ziara hiyo.Ziara hii imekuwa ya manufaa makubwa kwa kuwa imebaini changamoto kadhaa ambazo zikiachwa, athari ya viwanda hivi kwa Mkoa na Taifa haitaonekana. Kubwa zaidi ni kufanya kazi chini ya uwezo kutokana na ukosefu wa malighafi (matunda). Hili limebainika ni kutokana na kukosekana kiunganishi na wazalishaji kwa kuwa hawajui ni matunda ya aina gani na yenye ubora upi yanatakiwa. Katibu Tawala Mkoa ameelekeza wataalam wa kilimo zifanyike kila jitihada kuondoa pengo hili na kwa kuanzia ufanyike utambuzi wa wakulima wa maembe kwa mkoa wote wa Pwani ndani ya kipindi cha miezi 3 kuanzia August 2021.Halikadhalika viwanda viandae utaratibu wa kilimo cha mkataba ili washirikiane na wakulima kuzalisha mali ghafi na uhakika wa soko la mazao hayo kwenye viwanda husika.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %