0 0
Read Time:58 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 26,2021.

Ni ujinga kudhani kuwa Sheria za Nchi zipo kwa ajili ya watu fulani tu lakini Sheria hizo ugeuka kuwa “udikteta” zinapowakumba watu wengine!

Baada ya sherehe kubwa kutoka CDM baada ya kukamatwa kwa lengai Ole Sabaya na kusisitiza kuwa Rais Samia Hassan “ANAUPIGA MWINGI”, leo wameshasahau yote haya na kuanza kumwita Rais dikteta kisa kukamatwa kwa mwenyekiti wao!Hawaoni hata aibu!

Lazima tuwe tayari kukabiliana na upotoshaji huu wa makusudi unafanywa na CDM kwa kueneza propaganda Nje ya Nchi kwa lengo la kuharibu sura ya Rais na sura ya Taifa!Vijana wa CCM tunapaswa kuanza kupambana na propaganda hizi kwa lengo la kutetea utawala wa Sheria dhidi ya kikundi hiki ambacho kinajaribu kutengeneza mazingira ya kuwa “untouchable“.

Hii haikubaliki,Watanzania lazima tuungane na kusema hapana dhidi ya uhuni huu!Hapana!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan

Mwandishi kijana wa CCM,Makamu Rais Daruso-IJMC,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Vyuo Vikuu Saut & Tumaini Iringa,Ofisa zamani Idara ya Habari- Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani Chuo cha maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na Mtia nia wa Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %