

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 1,2021.
Andiko langu la leo asubuhi lilikuwa na jicho kali kuhusu jinsi kauli zetu wana CCM zinaweza zikaibomoa Serikali yetu,je,wamachinga wa Dar es salaam hasa eneo la mbagala, walichofanya leo inaweza kwamba ni matokeo ya “backup statement” kutoka kwa viongozi wangu wa Chama?
Contradicting statements kutoka katika Serikali dhidi ya Chama dola kwa vyovyote tusipokuwa makini zinaweza zikawasha hasira kwa makundi fulani dhidi ya Serikali yetu pasipo sababu za msingi!
Sisemi kwamba kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kile kilichotokea leo Mbagala na kile viongozi wangu wa ccm walichosema lakini pia sio vizuri kupuuza “hypothesis”hizi, naweza kuona kuwa inawezekana sana!
Machinga kote Nchini lazima wajue kuwa Serikali hipo na wakati wote hipo na kamwe wasije sehemu nyingine wakafanya hivyo!
Hatuwezi kuwa na wafanyabiashara ambao wanataka kufanya biashara popote mpaka barabarani na mitaani,hii haiwezekani na tusikubali iwezekane!
Ni ujinga sana kusema machinga wanafwata wateja!Mara zote duniani mteja ndio anafwata huduma hasa huduma za machinga ambazo ni bei Chee na rafiki kwa Watanzania wengi!Kutuambia kwamba sehemu fulani hakuna wateja ni uongo mkubwa!
Kamwe viongozi wangu wa ccm na Serikali ya Chama cha Mapinduzi isije ikasalimu amri kwa sababu yoyote.
Hii haikubaliki!viongozi tokeni maofisi kanusheni hoja za dhaifu za wamachinga kwamba biashara ndio inawafwata wateja kwani duniani kote, mteja ndio anafwata huduma/bidhaa!
+255784159968.








