0 0
Read Time:2 Minute, 29 Second
JICHO LA ULEDI

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
March 31,2022.

Sishangai kwanini kunakuwa na leadership dillema kiasi hiki ndani ya taasisi nyingi za Serikali kiasi kwamba inafika wakati kuna mambo mengi ya msingi hayaendi kwa viwango,spedi na wakati sahihi!

Mh.Rais Samia Suluhu Hassan amenukuliwa hivi karibuni akilalamika na kutilia shaka uwezo wa wateule wake katika nafasi wanazoshikilia maofisini katika maeneo mengi ya Nchi na katika ngazi mbalimbali!

“…unashangaa shirika halina bodi kwa miaka sita wakati maombi yote ya kuundwa kwa bodi hizo nilishapitisha zamani…….”.

“…mnakimbilia nafasi wakati hamuwezi kuzitumikia….”Mh. amesikika hivi karibuni!

Katibu Mkuu kiongozi, ndugu yangu Hussein Katanga, alipokuwa anaapishwa katika nafasi yake hapo mwaka jana, aliwahi kusema kuwa moja ya changamoto kubwa ya kuendesha shughuli za Serikali ni Nchini ni kukosekana kwa kitu alichokiita coordination ndani ya Serikali hasa kati ya taasisi moja na taasisi nyingine!

Ni bahati mbaya sana mamlaka za uteuzi uletewa watu ambao wakati wengine hawana sifa za msingi zaidi ya kupigiana pasi za hapa na pale hasa wakati wa teuzi hizi!

Mwaka jana tumeona jinsi wateule zaidi ya watatu, majina yao yalifutiliwa mbali muda mfupi baada ya kutangazwa na vyombo husika baada ya Mh RAIS kugundua janja janja fulani nadhani katika michakato ya uteuzi husika

Kibaya zaidi teuzi zetu sio tu kwamba zinapumbazwa na vyeti lakini pia zinapumbazwa na uccm kuliko uwezo!
Undugu kuliko uwezo na urafiki kuliko uwezo wa mtu!Siasa kuliko uwezo wa MTU!Tunataka nini?

Teuzi zetu pia zinajibana zenyewe kwenye kuangalia kwenye kapu moja la watumishi wa Umma tu, utadhani ni dhambi kuingiza mtanzania mwenye uwezo katika utumishi wa umma!Profesa Assad aliwahi kusema kuwa,nanukuuu;

“….karibu ya asilimia kubwa ya watumishi wa Umma hawana uwezo….”

SITAKI kukubaliana na Prof. Assad moja kwa moja lakini kwangu mimi naona kwamba, watumishi wa Umma wengi hawana “njaa” na “aggressiveness” ya maendeleo katika majukumu wayafanyayo ya kila siku hivyo, utumishi wa umma unakosa mambo makubwa matatu(I)Creativity(II)Spidi na (III)Quality

Kuna umuhimu mamlaka za uteuzi kuangalia uwezo wa wateule na historia zao kama tunataka kupiga hatua za haraka!Haiwezekani sifa ya kuwa mfano, KM,RAS, DED,DC au DAS ikawe kuwa kada wa CCM tu au mtumishi wa Umma na kigezo cha kuwa na elimu pekee yake!

Ifike kipindi tuangalie nje ya sifa za kawaida na kuamua kwenda mbali zaidi ya sifa za kawaida “routine qualifications”, mfano,(I)historia yako mteule huko nyuma na umefanya nini utokako?(II)Maono na matamanio yako mteule”vision” katika nafasi unayotaka kuteuliwa(III)Uadilifu wa mteule na mapenzi yake kwa Nchi yake(IV)kujitoa kwa mteule kabla ya uteuzi katika shughuli za kitaifa za maendeleo!

Sifa ya kuwa na hofu ya Mungu kwa wateule wetu ni muhimu sana ili kuweza kuzuia wizi na uporaji wa mali za Umma huko maofisini!

Nakubaliana na Mh. Rais na Mama yangu,Samia Suluhu Hassan kwamba teuzi zake zote kuanzia sasa anapaswa kuzicross- check sana na kamwe hasimwamini mtu!Tunawapa nafasi baadhi ya watu ambao viwango vyao sometimes ni very questionable!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %