0 0
Read Time:54 Second

Na Harid Mkali

UK

WU®Media PRODUCTION

# Ubora wa watu wanaoisimamia Katiba yoyote duniani ni bora zaidi kuliko ubora wa Katiba yenyewe. Ndiyo kusema Katiba mzuri ni bure ghali iwapo viongozi si bora.
Hii ni sawa na kuwa na “guided missile” ambayo ipo kwenye mikono ya mtu ambaye ni “misguided”.

# Katika Marais ambao tumekuwa nao Tanzania tangu uhuru, hayupo ambaye katika muhula wa miaka mitano alileta miradi na huduma kubwa na muhimu kumpita Dr. Magufuli. Hayupo. Je, Magufuli alitumia Katiba Mpya?

# Chama cha Chadema, kilianza na wabunge wa kuchaguliwa watano. Wakati kinakwenda kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 walikuwa na Wabunge wa kuchaguliwa zaidi ya 100. Je, ilikuwepo Katiba Mpya? Je, kulikuwa na Tume za Uchaguzi Mpya katika muda huo?

Hivyo basi, ninakubaliana na kwa kutolipa kipaumbele hili suala la Katiba Mpya. Mama yupo sahihi.

Kuhusu Afrika ya Kusini na Kenya, yamkini ni mifano bora ya Katiba ambazo si mzuri; na mengi ya matatizo yao yanatokana na mchanganyiko wa: (a) udhaifu wa Katiba na (b) udhaifu wa ubinafsi uliokithiri wa Viongozi wao.

mkali@live.co.uk.
30/03/2022.

Happy
Happy
100 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %