0 0
Read Time:2 Minute, 32 Second

Ubunifu na uchapakazi wake

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
April 20,2022.

Unaweza kusema hakuna namna tena zaidi ya kumpenda tu,hakuna namna tena zaidi ya kuikubali tu akili yake kubwa na hakuna namna tena zaidi ya kukiri tu kuwa filamu ya Roya Tour Tanzania Edition inaweza kutuletea fedha yote ya kujengea kipande cha SGR chote cha makotopola mpaka Tabora ndani ya mwaka mmoja tu!

Uzinduzi pekee wa pale Jijini New York,achana na miji mingine ya Nchi ya Marekani, unaweza kukupa picha ya ukubwa na utajiri wa filamu hii ya kibabe toka Nchini Tanzania,Nchi ya pili duniani baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vingi vya “kishua”!Unabisha?

Royal Tour Tanzania Edition katika siku yake ya kwanza ya uzinduzi na sio sokoni,imeweza kurushwa na vituo vya habari 300 Marekani,imetazamwa na watu karibia Bilioni moja duniani na ndio imekuwa habari kubwa leo katika magazeti na majarida mengi ya Marekani hasa ya utalii na yasio ya utalii!Unabishaa?

Mahojiano pekee ya jana kati ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na “The Superdupa Producer” Peter Greenberg,wakati wa uzinduzi wa filamu ile, yaliweza kuangaliwa angalau na watanzania wapatao milioni 15 ndani ya nusu siku ya jana pekee yake baada ya kuachiwa hewani!Unabishaa?

MH.RAIS SAMIA “FUNIKA BOVU”!

I.Dunia na hasa watu wa marekani wamshangaa kuhusu uwezo wa Rais wangu Samia wa kujibu maswali ya kingereza kwa ufasaha na utulivu wa viwango vya juu!

“….ooh,I admire you madam President..,what can you tell the gals who want to be like you?”.

II.Aweza kupangua maswali magumu na ya mitego kuhusu utaliii wetu kiasi kwamba angekosea kujibu tu, tayari watalii wetu wangeanza kuwa na wasiwasi kuhusu filamu yetu na ukubwa wa utalii wetu!

“..when is the right time to visit Tanzania ?”.aliuliza na Binti mmoja wa kimarekani.

Mama ndio hapo akaanza kuteleza,utadhani sio mswahili wa Zanzibar!

“…I think is June &July,but when you want to see the Serengeti migration then it is August….but you can came all the time,…we can even stop the rain for youuuu….”.

Ukumbi mzima wamarekani wakawa hawana mbavu kwa kichekoo,Unabishaa?

III.Mama Samia hakuwa mjinga kutaka kuiçheza filamu yake “The Royal Tour Tanzania Edítion”yeye mwenyewe,angeweza kumpa hata Mzee wangu Mizengo Pinda aicheze!Unajua alichokuwa anataka “kuiject” ndani ya filamu ile?Akili kubwa kabisa ya mwanamama kutoka Tanzania!

Sisi kwa sasa ni miongoni mwa mataifa machache ya mfano duniani kote katika mambo MAKUBWA mawili(I) ukubwa na ukomavu wa demokrasia yetu hasa wakati wa makabidhiano ya madaraka kutoka awamu ya tano kwenda awamu ya SITA bila kelele tena kutoka jinsia moja kwenda jinsia nyingine,Unabishaa?(ii)sisi Tanzania ni miongoni mwa Nchi chache duniani ambàzo zimeweka historia ya pekee kwa kuongozwa kwanza na makamu wa Rais na baadae Rais mwanamke!Unabisha?

Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuthibitisha usemi wake kwamba na hapa namnukuu kidogooo!

“…nitaitumia kila fursa nitakayoiona duniani kwa ajili ya kuwaletea maendeleo watanzania hawa…”.

Ndio tumeanza kuokota fursa moja moja,moja moja na labda tukutane mwaka 2025 tuone!

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %