
Na Kagutta Maulidi
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amekutana na Watanzania wanaoishi Marekani.
Rais Samia yupo Marekani kwenye ziara ya kikazi,ambapo tangu amefika amekutana na Makamu wa Rais wa Marekani , taasisi mbalimbali za kimataifa na wafanya biashara wakubwa na wewekezaji. Mh Rais pia alishiriki uzinduzi wa The Royal Tour uliofanyika New York na Los Angeles California.
Rais Samia akiongea na Watanzania hao aliwaeleza Hali ya kisiasa nchini inavyokwenda vizuri katika kuimarisha Demokrasia ya vyama vya siasa kwa ujumla. Pia alikiri kukutana na kuona mabango ya baadhi ya Watanzania waliodhamiria kufikisha ujumbe kwa Mh Rais kwa maandamano ya Amani yaliyofanyika nje ya Ubalozi wa Tanzania. Rais pia aliwatoa shaka Diaspora husani suala la hadhi maalumu ambalo lipo kwenye mchakato ambao unaendelea kuhusisha wadau wa Diaspora kuchangia maoni yao,akizungumza na Watanzania wanaoishi Nchini Marekani Jijini Washington DC aliwaambia kuwa suala la urai pacha kwa sasa halipo mezani,isipokuwa ni hadhi maalumu itakayo wapa Diaspora fursa zaidi na haki kama wazawa.
















