0 0
Read Time:1 Minute, 32 Second

ITALY -TANZANIA BUSINESS AND INVESTMENT FORUM 2022.

Na Mwandishi wetu

Dar Es Salaam TANZANIA

WU® MEDIA

Balozi wa Italy nchini Tanzania (L’Ambasciatore) Marco Lombardi amekutana jioni ya Leo kwenye makazi yake Jijini Dar Es Salaam na wadau mbalimbali wa biashara waliohudhuria kongamano lilofanyika Zanzibar na DarEs Salaam.

Balozi Marco Lombardi akiongea na wadau wa biashara kwenye makazi yake Jijini Dar Es Salaam

Katika ghafla hiyo ya chakula Cha jioni pia ilihudhuriwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mh. Mahamoud Thabit Kombo, Mabalozi hao ambao wamekuwa akishirikiana Sana kwenye masuala mbalimbali ya kidiplomasia na hasa kwenye Uchumi,walisisitiza na kuwataka wadau Kujiongeza zaidi katika kuzitumia fursa za pande zote mbili yaani Italy na Tanzania. Balozi wa Italy nchini Tanzania Mh. Marco Lombardi amewataka wawekezaji wa italia kutumia fursa zilizopo Tanzania kwenye sekta mbalimbali na kutumia fursa ya misamaha ya Kodi kwa wawekezaji .

Balozi Mahamoud Thabit Kombo alimsisitiza Balozi mwezie kutoa fursa za visa kwa wafanya biashara wa Tanzania ambao wanahitaji kwenda Italy kutafuta fursa zaidi.

Balozi Mahamoud Thabit Kombo akiongea na wadau kwenye ghafla iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Italy Nchini Tanzania Mh. Marco Lombardi.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mh. Mahamoud Thabit Kombo akiwa na mkewe katika ghafla iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Italy Jijini Dar Es Salaam Leo jioni.
Madam Eva Joseph Nangela (c) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Genova nchini Italy, mmoja wa Diaspora waliohudhuria kongamano la Italy – Tanzania Business and Investment Forum. Diaspora wamejiongeza katika kuzichangamkia fursa za kibiashara na kutoa mchango wao katika kutafuta wawekezaji wa kitaliani kuwekeza nchini Tanzania.
Mama Balozi
(c) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Genova Italy Bi Eva Joseph Nangela akiwa na Diaspora wenzie waliohudhuria Kongamano la Italy -Tanzania Business and Investment Forum, lililofanyika Zanzibar na Dar Es Salaam TANZANIA.
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %