0 0
Read Time:53 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

By: Dr. Abbasi, KM, WUSM

jamhuriyawapambanaji: Moja ya mafanikio makubwa ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka kwa Walemavu, Tembo Warriors, ukiacha kufika robo fainali na sasa imeingiza nchi katika mataifa bora 8 duniani kwa mchezo huo, ni uharaka na maajabu ya mafanikio yao, hamasa kubwa ya Watanzania wa Uturuki na sasa duniani sehemu mbali mbali inazungumzwa Tembo Warriors.

Hapa Uturuki viongozi, wachezaji wa nchi mbalimbali hawakosekani katika mechi za Tembo Warriors, mawakala wa wachezaji kwa ajili ya ligi mbalimbali kubwa za mchezo huu hawakauki kila mwisho wa mechi kujazana uwanjani kuzungumza na wachezaji wa Tembo Warriors (kadhaa wapya ukiacha wale wanne walioko Ligi Kuu ya Ututuki, nao wameshapata timu tayari).

Simon Baker alipata ajali miaka ya 2000 akiwa site ya ujenzi na leo ni mmoja wa watu mashuhuri duniani akichagia mchezo huu kwa mataifa mbalimnali amewasiliana nasi kuwa anakuja tena Tanzania kwa programu zaidi lakini kubwa anawakubali sana Tembo Warriors, anawakubali sana wadau wa mchezo huu Tanzania na amenambia anakubali sana sapoti ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchezo huu.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %