
TEMBO WORRIORS YAPANDA DARAJA DUNI Tanzania Yaitwanga Italia Kombe la Dunia Walemavu, Yashika Nafasi ya 7 Ubora Duniani:
Tanzania Yaitwanga Italia Kombe la Dunia Walemavu, Yashika Nafasi ya 7 Ubora Duniani:
Timu ya Taifa ya Tanzania, Tembo Warriors, baada ya kufika robo fainali ya Fainali za Kombe la Dunia la Soka kwa Walemavu, leo imemaliza mechi za kuwekwa katika viwango vya ubora duniani kwa kuitandika Timu ya Taifa ya Italia kwa mabao 2-0 katika mechi kali iliyochezwa mjini Istanbul, Uturuki.
Fainali ya mashindano hayo inachezwa usiku huu mjini hapa na Tembo Warriors inarejea nyumbani kesho na jumatatu mchana inatarajiwa kupokewa na maelfu ya mashabiki wa michezo.
Timu tatu za Afrika; Angola, Morocco na Tanzania ndio pekee zimeingia 10 Bora ya Orodha ya Viwango vya Shirikisho la Soka kwa Walemavu Duniani (Waff). Hongera Tembo Warriors, Hongera Tanzania.
.








