
COORDINATION FAILURE NDIO UGONJWA MKUBWA KWENYE INJINI YETU YA MAENDELEO!
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
October 16,2022.
Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Mzee wangu hayati John Pombe Magufuli alikuwa analazimika kila siku kutaka kuizunguka Tanzania huku akikutana na madudu mengi katika Utumishi wa Umma na baadae ikabidi aje na style ya kutumbua Watumishi wa Umma hadharani, mchana kweupe,Ile unajua inaitwaje?Ile inaitwa kwa kizungu ni “Coordination failure”!
Kwanini hayati JPM alitaka awepo kila sehemu, ilikuwa anapambana kutaka kuiziba kwa haraka hiyo “Coordination failure”,bahati nzuri alishaanza kufanikiwa!
Rais wa awamu ya Sita Mama yangu Samia Suluhu Hassan wakati anamwapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Kaka yangu Mh Balozi Katanga nakumbuka alimwagiza kwenda kushugulikia tatizo la “Coordination failure” katika Utumishi wa Umma!
Miaka miwili sasa tatizo linaonekana lipo pale pale!Kuna sehemu Msimamizi Mkuu wa Utumishi wa Umma KMK Balozi Katanga anatakiwa kupafix!Papo!

Mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan jana akiwa katika Sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru Mkoani Kagera juzi, alisikikia akizitaja taasisi nyeti muhimu mbili yaani Takukuru na ZAECA na kuzionya kuwa zinatakiwa kujikagua zenyewe ndani kabla ya kukagua wengine!The some problem of Coordination Failure”.
Kwa kiswahili rahisi “government activities coordination failure” ni ile hali ya kushindwa kwa either taasisi,mifumo,watu au dhamira,dira katika Taifa kuweza kuongea lugha moja Mfano,Ngoma inayopigwa Ikulu ya Magogoni/Chamwino na Mh Rais, Mama Samia sio ndio ambayo inayochezwa Mikoani na Wateule wake,hata Watumishi wa Umma na hata Wananchi wa kawaida!Hawechezi ngoma yenye korasi moja!
Jeshini kuna kitu kinaitwa chain of command!Dhana ya Chain of command jeshini haipo kwenye makaratasi tu lakini uenda pamoja na (I)Nidhamu na Uzalendo,(II)Utii kwa Viongozi wa Juu (III)Utayari wa kufuata maelekezo na kuyatekeleza kwa usahihi wa viwango vya juu! In order coordination to function well,lazima kuwe na nguzo mbili kuu yaani “Reward and Punishment”!
Kwahiyo Coordination failure ni matokeo ya kutokuwepo mifumo miwili IMARA kwenye Uongozi ambayo ni (Reward & Punishment).Sijui naeleweka!Somo jepesi kabisa la Uongozi najaribu kulitoa hapa!”Basics of Leadership”!
Roho ya ufanisi wa Serikali yoyote duniani utegemea sana ujuzi Serikali yenyewe wa kutengeneza vitu vifuatavyo;(I)a Coordinated and shared national vision opely known to every body from up to bottom and bottom-up (II)Pia uwezo wa Serikali yenyewe kuweza kutengeneza “Coordinated Institutions (III)na zaidi ni uwezo wa wateule wa Mh Rais kujua kuwa wanakuja kuyatumikia kwa dhati maono,matamanio,dhamira na dira ya Mh Rais kwanza!
Serikali inayojua jinsi ya “kuyaenject” mambo hayo makubwa ya msingi MATATU hakika itakuwa imekwepa kuingia katika mtego mgumu kutoka wa “Coordination failure”!
Ni aibu mpaka leo unakuta Waziri/Wizara haijui kuwa mdau wake namba moja katika kumtekelezea mipango ya Kilimo kwa mfano ni RC,DC,DED, Diwani,na hata Mwenyekiti wa kitongoji!Mipango ya WIZARA Mfano ya Kilimo ilipaswa ibuniwe na Tamisemi pamoja na WIZARA!
Mfano,mpaka juzi WIZARA za Serikali moja ya CCM, zilikuwa bado hazina wazo la kukutana pamoja na kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji mpaka Mamlaka za Uteuzi zilipotoa maelekezo ya haraka na kuwataka Mawaziri karibia nane wa Kisekta kuizunguka Tanzania angalau kuweza kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji!Hakuna kingine ni “lack of Coordination” tu!
Je,watumishi wa taasisi kama Takukuru na Watumishi wa taasisi kama ya ZAECA, ni kwa kiasi gani wameishiba Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, mwaka 2025 ,Mpango wa Maendeleo ya Taifa na hata Mipango ya kibajeti ya kila Mwaka?
Serikali zangu za CCM mpaka sasa,Je, zimewahi au kwa kiasi gani zimekuwa zikiwashirikisha angalau Maofisa wa Takukuru na ZAECA mfano,zinapokuja fedha za maendeleo”UVIKO- 19,Fedha za Madarasa na zingine nyingi angalau zinapofika huku Halmashauri angalau na wao tuwape miongozo,BOQ na terms zingine kuhusu matumizi ya fedha hizo kabla mradi haujaanza kutekelezwa!Kama tunafanya hivyo basi big heko awamu ya Sita!
Moja ya kitu ambacho kinaweza kutuchelewesha sana Rais wangu na Mama yangu, SAMIA kufikia malengo yetu na malengo ya Taifa katika kuwaletea watu wetu maendeleo basi itakuwa ni uwepo wa Coordination failure!
Kwa sababu hizo hizo kuna Takukuru na ZAECA inafika wakati wanadhani fedha na miradi ile ya local government labda ni miradi ya RCs,DCs au DEDs lakini miradi ya fedha inayotoka Serikali kuu moja kwa moja ndiyo wanapaswa kudeal nayo!Ulkitaka kujua kuwa Ndugu zangu wa Takukuru au ndugu zangu wa ZAECA,kwamba hawana taarifa za kutosha kuhusu miradi husika ni pale kila siku na mara nyingi wanapochukua maelekezo toka kwa Mawaziri, MaRCs na MaDCs ya kukamata watu wakiwa “site”!Unajiuliza,Ndugu zangu wa Takukuru walikuwa wapi mpaka yote yanatokea haya?
Mwandishi ni kijana na kada wa CCM,Makamu Rais wa zamani, Daruso-IJMC,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha, Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut na Tumaini Universities na Mtia Nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255746726484.








