
Miaka 23 bila ya Mwalimu!
Kuhusu Umoja na Amani
Novemba 14, 1965 Mwalimu Nyerere alifungua mkutanao mkuu wa kwanza wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo Baba wa Taifa aliwahusia wanawake wote umuhimu wa kuwa na umoja na serikali yake ilivyokuwa inajitahidi kuondoa tofauti zilizokuwapo miongoni mwa wananchi.
Alisema, “Tunayo mazoea viongozi. Sisi viongozi wetu tuliozoea tangu mwaka 1954 ni viongozi katika kupingana na makundi, sasa ninachowaonya kina mama na viongozi wote wa Tanzania, nawaomba lazima kama nchi imegeuka, nchi hii ina umoja.
Hakuna hata moja katika Afrika ina umoja kuzidi Tanzania. Hakuna hata moja. Anayejua nchi moja katika Afrika yenye umoja wa hiyari zaidi kuliko ya Tanzania aniambie. Ziko nchi zina umoja wa bunduki. Hapa bunduki ziko wapi? Tanzania ina umoja. Watu wanasikilizana. Watu wanakuja wanashangaa. Kitu kimoja kinachoshangaza dunia ni umoja. Ndicho tulicho nacho vingine hatuna”.
Francis Daudi
14-10-22
BAADHI YA MAFANIKIO MAKUBWA YA BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE:

1) TAZARA (SGR ya Kwanza Afrika Mashariki na Kati) aliijenga na mwenzie Rais Kenneth Kaunda wa Zambia.
2) Reli ya Singida – Manyoni.
3) Kiwanda cha Nyuzi Tabora.
4) Viwanda kama 11 vya Korosho nchini.
5) Viwanda kama 11 vya Nguo nchini. Mfano: Mwatex, Urafiki, Ubungo Garments, n.k.
6) Mabwawa ya Kufua Umeme ya Kidatu, Mtera, Kihansi, n.k.
7) Meli Kubwa Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika.
8) Shirika la Ndege la ATC lililokuwa na Ndege 14.
9) Vyuo Vikuu. Chuo Kikuu cha DSM na Chuo Kikuu cha Mzumbe.
10) Vyuo Vikuu vya Ufundi Nchi nzima. Mfano: DSM Technical College.
11) Shule za Sekondari za Ufundi. Mfano: Shule ya Sekondari ya Milambo.
12) Vyuo wa Tiba.
13) Vyuo vya Ualimu.
14) Kuimarisha Mabasi ya Railway.
15) Kampuni ya Usafiri ya Jiji la DSM (UDA).
16) Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA).
17) Ranchi Kubwa za Taifa za Mifugo. Mfano: Ranchi ya Taifa ya Ruvu, Ranchi ya Taifa ya Morogoro, Ranchi ya Taifa ya Kongwa, n.k.
18) Mbuga za Wanyama 10.
19) Vyuo Viliwalipa Wanafunzi Fedha za Matumizi.
20) Wanafunzi wa Sekondari (Boarding Schools) Serikali ilikuwa inawasafirisha bure kutoka Shuleni kwenda Nyumbani na kutoka Nyumbani kwenda Shuleni. Walikuwa wanapewa “Warrants”.
21) Elimu ya Watu Wazima. Zaidi ya 95% ya Watanzania walikuwa wanajua Kusoma na Kuandika. Na.1 Afrika.
22) Hospitali Kubwa za Rufaa Nchini. Mfano: Muhimbili, Bugando, KCMC, n.k.
23) Mahoteli MAKUBWA ya Kitalii. Mfano: Kilimanjaro Hotel, Embassy Hotel, Mawenzi Hotel, Bahari Beach Hotel, Mount Meru Hotel, Mwanza Hotel, n.k.
24) Vyuo Vikubwa vya Kilimo. Mfano: Chuo cha Uyole, Chuo cha Naliendele, Chuo cha Ilonga, Chuo cha Ukiriguru, n.k.
25) Viwanda vya Vifaa vya Umeme.
26) Viwanda vya Baiskeli.
27) Viwanda vya Matairi.
28) Viwanda vya Vipuri vya Magari.
29) Viwanda vya Radio za Phillips na National.
30) Viwanda vya Betri.
31) Kiwanda cha Magari cha Nyumbu.
32) Kiwanda cha Malori ya Scania.
33) Viwanda vya Kuchambua Pamba (Ginneries).
34) Elimu Bure kuanzia Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu, Vyuo vya Diploma na Vyuo vinavyotoa Vyeti. Madaftari bure, Kalamu bure, Vifaa vyote vya Shule bure, Matibabu bure na Chakula bure.
35) Huduma za Afya bure kabisa! Kumuona Daktari bure, Vipimo vyote bure, Dawa bure, Maji ya Kunywea Dawa bure, Sindano bure, Kufungwa Vidonda bure, Upasuaji bure na Kulazwa bure.
36) Mafanikio Makubwa Katika Utamaduni na Michezo. Mfano: Filbert Bayi alichukua Ubingwa wa Dunia Mbio Ndefu 1,500m.
37) Vikundi Vikubwa vya Ngoma. Mifano ya Magwiji Wakubwa wa Ngoma za Kienyeji ni Mzee Makongoro, Mzee Mwinamila, Mzee Morris (Kipofu aliyekuwa anapiga Ngoma 10), n.k.
38) Mzee Mayagiro na Bendi ya Polisi.
39) Bendi za Muziki wa Dansi karibu kila Mkoa.
40) Bendi Maarufu za Muziki wa Dansi Kwenye Mashirika ya Umma. Mfano: Urafiki Jazz Band, Bima Jazz Band, n.k.
41) Bendi Maarufu ya Wafanyakazi. NUTA Jazz Band. Msondo Ngoma.
42) Bendi Maarufu za Muziki wa Dansi Polisi na Jeshini. Mfano: Kimulimuli Jazz Band.
43) Michezo Mashuleni. Mfano: Mashindano ya UMISETA yaliyoshindanisha Shule za Sekondari Nchi nzima.
44) Mpira wa Miguu ulikuwa juu kwa Vilabu, Wachezaji na Timu ya Taifa. Na Michezo mingine.
45) Mashindano ya Kombe la Taifa yalishindanisha Mikoa yote Nchini kila mwaka.
46) Vyama Vikubwa vya Ushirika wa Mazao Makubwa. Mfano: Nyanza, Shireku, n.k.
47) Alijenga Umoja Imara wa Kitaifa. Kiswahili kilitumika Kujenga Umoja Imara sana.
48) Hakujenga Nyumba. Alikopeshwa na aliulipa Mkopo wake wote kidogokidogo toka Mshahara wake mdogo. Nyumba ya Butiama alijengewa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kama Zawadi baada ya Kustaafu.
49) Alipokufa iligundulika kwamba alikuwa na Akaunti ya Benki moja tu Nchini (NBC) na haikuwa na hata senti 5. Hakika Mwalimu Nyerere alikuwa Mtakatifu.
50) Aliheshimiwa Duniani kote. Na Nchi yetu pia.
51) Alikuwa Mwenyekiti wa Nchi za Mstari wa Mbele (Frontline States).
52) Aliendesha Kambi za Wapigania Uhuru za Kongwa, Morogoro, n.k. kwa Gharama Kubwa za Nchi yetu. Aliwapa Hifadhi Wapigania Uhuru toka Msumbiji, Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, n.k.
53) Alikuwa Mwanafalsafa aliyeheshimiwa sana Duniani. Hotuba na Vitabu vyake vilikuwa, na vinaendelea kuwa, vivutio vikubwa Tanzania, Afrika na Dunia nzima.
54) Aliandika vitabu zaidi ya 20.
55) Bodi za Mazao Makubwa Nchini. Mfano: Bodi ya Pamba, Bodi ya Tumbaku, Bodi ya Korosho, Bodi ya Kahawa, n.k.
56) Alianzisha GAPEX.
57) Tanzania Elimu Supplies (TES).
58) Tanzania Publishing House (TBH).
59) TAFICO.
60) Chuo cha Uvuvi Mbegani.
61) Vyuo vya Utalii na Wanyamapori.
62) Vyuo vya Kilimo vya Tumbi, Uyole, n.k.
63) Viwanda vya Kahawa.
64) Secretarial Colleges DSM na Tabora.
65) Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO).
66) Bwawa la Mindu.
67) Kuimarisha Kiswahili kuwa Lugha ya Taifa.
68) Alipiga Vita na Hakuruhusu kabisa Ukabila.
69) Alipiga Vita na Hakuruhusu kabisa Rushwa.
70) Mashamba Makubwa ya Mpunga. Mfano: Mbarali na Dakawa.
71) Kiwanda cha Nyama cha Tanganyika Packers.
72) Kiwanda cha Coca-Cola, Shinyanga.
73) Kiwanda cha Saruji.
74) Mashamba ya Zabibu.
75) Kiwanda cha Kutengeneza Mvinyo cha Dodoma. Dodoma Wine.
76) MOPROCO.
77) Morogoro Canvas Mill. Kikubwa kuliko vyote Afrika.
78) Kiwanda cha Sigara.
79) Kiwanda cha Karatasi cha Mgololo. Kikubwa kuliko vyote Afrika .
80) Kiwanda cha Bia (Tanzania Breweries).
81) Kilimo cha Matunda Tanga.
82) Chuo cha Posta.
83) Chuo cha Kodi.
84) Chuo cha Sukari.
85) Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya.
86) Kiwanda cha Zana za Kilimo (UFI), DSM.
87) Shilingi iliyowahi kuwa na thamani kubwa kukaribiana na Dola ya Marekani na Pauni ya Uingereza.
88) Kiwanda cha Kibuku.
89) Kiwanda cha Konyagi.
90) MECCO.
91) Kiwanda cha Sigara
92) Kiwanda cha Kuchapa Vitabu na Magazeti ya Serikali (Kiuta).
93) Kampuni ya Fenicha.
94) Kiwanda cha Mazuria.
95) Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
96) State Transport Corporation (STC).
97) Shirika la Utalii la Taifa (TTC).
98) Shirika la Habari Tanzania (SHT).
99) Shirika la Posta na Simu.
100) TANGOLD.
101) Cocabs.
102) Wakala wa Meli wa Taifa (NASACO).
103) Mamlaka ya Bandari (TPA).
104) Shirika la Reli (TRC).
105) Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
106) Vita vya Kagera. Alimtandika Dikteta Nduli Iddi Amin wa Uganda na kuwakomboa Waganda toka kwenye Utawala Dhalimu wa Dikteta huyo.
107) Alituletea Uhuru wa Tanganyika tarehe 09.12.1961.
108) Alisaidia kuzikomboa Nchi za Kusini mwa Afrika. Mfano: Msumbiji, Afrika Kusini, Angola, Namibia, Zimbabwe, n.k.
109) Muasisi wa Muungano wa Tanzania na Zanzibar akishirikiana na Marehemu Rais Abeid Amani Karume tarehe 26.04.1964.
110) Muasisi wa Muungano wa TANU na Afro Shiraz Party kuunda CCM tarehe 07.02.1977.
111) Alikuwa tayari kuzisubiri Kenya na Uganda zipate Uhuru ili tuungane nao tuwe Nchi moja.
112) Alijenga UZALENDO.
113) Hadi anang’atuka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliacha Viwanda vya Umma kama 500 na Mashirika ya Umma mengi sana, achilia mbali Kampuni za Watu Binafsi na Viwanda.
114) Na mengine mengi!
115) Na mengine mengi sana!
AHSANTE SANA MWALIMU! TUTAKUKUMBUKA DAIMA BABA WA TAIFA! MUNGU AWE NAWE! AMINA!
KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 2022.








