
Na
Zain Hamza
Mwanadiaspora
Washington
Hadhi maalumu ina faida nyingi kuliko uraia pacha, kwa taifa
Hadhi maalumu ina faida nyingi kuliko uraia pacha, sio kwa taifa tu, hata kwa wanadiaspora wenyewe.
Hadhi Maalumu = haki za uraia wa Tanzania kwa wazawa wa Tanzania na vizazi vyao.
Uraia pacha = uraia wa Tanzania kwa raia wa nchi zote duniani.
Hadhi maalumu inalinda uraia wa nje wa mwanadiaspora kama ulivyo, na anapata haki za uraia wa Tanzania kasoro ushiriki wa kwenye siasa.
Uraia pacha unampunguzia mwanadiaspora haki za uraia katika nchi zote mbili kama ifuatavyo;
- Hawezi kupata kazi za kuaminika katika serikali zote mbili.
-Hawezi kupata uongozi wa siasa katika nchi zote mbili.
-Anaweza kulipishwa kodi nchi zote mbili.
-Anaweza kuitwa jeshini nchi zote mbili.
-Anakosa hifadhi na kinga ya uraia wake wa nje akiwa Tanzania .
- Ana bughudha ya kutumia na kuzihudumia paspoti mbili.
- Anabeba matatizo ya nchi zote mbili. Wakifungiwa watanzania amefungiwa na yeye, wakifungiwa wamarekani amefungiwa na yeye.
- Na akigonganisha sheria au akivunja sheria ni rahisi mno kufutiwa uraia wake wa nje akabakiziwa na uraia wa Tanzania.
Watu wa uraia pacha hata wakisema wanaomba uraia pacha kwa wazawa, wanajidanganya tu;
- Kuna wageni watakaochukua uraia pacha kwa kutumia ndoa.
- Kuna matajiri wa kitanzania wenye asili ya nchi za nje hawatazuilika kuchukua uraia pacha na kwao kwa asili.
Mwisho wa siku wanadiaspora waliopigania uraia pacha na mishahara midogo ya nchi za nje watajikuta wanagombea ununuzi au umiliki wa ardhi na matajiri kutoka nchi jirani kama Kenya au watanzania matajiri wenye asili ya nchi za kigeni na wenye uraia pacha wa kihalali. Na wote hao watakuwa na haki za uraia sawasawa na yeye.
Halina siri hili wanadiaspora hawatakuwa na uwezo wa kupambana matajiri watakaochukua uraia pacha.
Kwa mwanadiaspora kuchagua uraia pacha na kukataa hadhi maalumu ni sawa na kujipunja chenji dukani.
Special status considered for Tanzanians in diaspora READ









