George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
October 20,2022.
THE ONLY CAME BACK WAY YA UPINZANI KWA SASA NI KUAMBATANA NA MH.SAMIA KWANZA!
JICHO LA ULEDI LAUANGALIA UPINZANI
Kwa Wanasiasa Wakomavu kama Ndugu yangu ZITTO ZUBERI KABWE wanaona kabjsa kwamba there is no way kwa sasa ya kuweza kupambana na Mama Samia na ukamshinda hasa kuelekea Mwaka 2025!Sababu zipo wazi kabisa kuhusu ukweli huu!
Moja ya sababu ni kwamba baada ya miaka karibia sita ya vyama vya wapinzani kutokufanya siasa za majukwani,ni wazi kwamba havina baseline ya kuanzia kufanya siasa za ushindani!Pili,wakati Mama Samia anauza kila siku miradi ya maendeleo kwa Wananchi wake ,wenyewe upinzani watakuja kuuza nini wakipewa jukwaa kwa sasa hivi?They will sell us propaganda tu!
Kwa wakati huu vyama vya UPINZANI havipaswi kuanza kuwaza kutafuta haki ya kufanya Mikutano ya hadhara,Strategists wazuri angewaambia kwamba huu ni wakati wao adhimu kabisa wa kufanya kitu kinaitwa”reorg” au Political re-orientation!
Kwenye Ulimwengu wa mpira wa miguu, unapokutana na gaint, wewe underdog unatakiwa umuache giant acheze kwanza!Mara zote underdog anapoingia uwanjani anatafuta matokeo ya aina mbili tu,moja ni kupunguza magori mengi,lakini Mungu akijalia hata kudraw au sare kwa underdog inakuwa mnamtosha kabisa!
Vyama vya Upinzani lazima vijue kufanya kitu kinaitwa”ground appreciation” kwanza kwa kukubali kuwa Mh Samia Suluhu Hassan na CCM kwa sasa ni giant sana kwao!La muhimu zaidi kwao kwa sasa ni kutafuta mambo makubwa mawili kwanza;
I.Angalau kwa sasa iwe ni kujaribu kuzipunguza kura za CCM za nafasi ya Urais,wabunge na Madiwani wa CCM katika UCHAGUZI wa Mwaka 2025 angalau kwa asilimia fulani!
II.Pili ni kutafuta Platform ya angalau kupata viti vya Ubunge na Madiwani kwanza kwa mwaka 2025 angalau katika baadhi ya maeneo ambayo wanaamini wana nguvu na sio katika kila maeneo Nchini!
Moja ya kosa kubwa ambalo wapinzani mtakuwa mnafanya ni kumuona Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa,Mh Mama Samia Suluhu Hassan ni size yenu na kudhani kwamba eti wakati wowote mnaweza kumvimbia!”kutia timu”!
Kwenye uwanja wa medani vikosi pinzani kupitia kamanda wao vinaweza kufanya kitu kinaitwa”tactical withdraw” sio kwa sababu vikosi vyako vimepigwa na adui, lahasha bali ni kwa sababu makamanda wanadhani kuendelea kimuengage adui kwa wakati huo kunaweza kuwaletea madhara zaidi na kuongeza casualties!
Moja ya Principle inayotumika katika kufanya maamuzi ya kuendelea na vita au lah kwa Kamanda ili kuweza kupunguza madhara wakati wa vita kwa vikosi vyake ni matumizi ya kitu kinaitwa “ground appreciation”!
Ni uwezo wa kamanda kusoma kwa haraka madhaifu na UBORA wake dhidi ya UBORA WA adui na Kamanda kuweza kupima na kufanya maamuzi ya kusimamisha vita au kuendelea na vita kwa lengo la kupunguza madhara na hata kupunguza matumizi ya rasilimali vita yasio na maana”tactical withdraw”!Somo rahisi kabisa la mpango vita!
Vyama vya UPINZANI kwa sasa lazima viwe na strategists wa kuishauri jinsi gani ya kufanya “Political deployment” kuelekea mwaka wa uchaguzi 2025!Moja ya kosa kubwa mnalopaswa kuachana nalo ni kudhani Tundu Antipas Lissu anajua kila kitu kuhusu strategia ya siasa!CCM inashinda Uchaguzi wakati wote si kwa sababu ya kudhani wanaiba kura lahasha,bali CCM inajua kuwatumia vizuri strategists wake katika kuchora mipango na ramani za siasa na ndio maana Kanali Mstaafu Lubinga na Kanali Mstaafu Kinana wapo Lumumba mpaka leo!
Uwanja wa Siasa ni kama Uwanja wa vita tu,tofauti yake Uwanja wa Medani unahusisha risasi na makombora”exchange of fire” lakini uwanja wa siasa unahusisha
“Exchange of ” sera na maono ya pande mbili!Angalau kuweza kushindana na CCM kwa sasa, mnahitaji kujua mambo haya!
Dalili ni wazi kabisa kuwa Mh Mama Samia Suluhu Hassan “ameshawapiga” asubuhi na mapema kabisa!Icheki ziara yake ya MBEYA IRINGA,NJOMBE,KAGERA, GEITA na KIGOMA zilivyobasti!Just appreciate kwamba huyu Mama Samia ni GIANT sana kwenu kwa 2025!
Mwandishi ni Mwalimu,Makamu wa Rais zamani, Daruso- -IJMC,Ofisa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Kadeti zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha, Mhadhiri Msaidizi zamani,Saut na Tumaini Universities!
+255746726484.