Na Mwandishi wetu. WU® MEDIA
Abbia Maswi ni msichana wa Kitanzania alipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya kwanza ya Mission Beauty yaliyo malizika mwezi disemba 2021. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na kuonyesha live kwenye Runinga ya Taifa inayojukikana kama Rai due, Abbia alishinda katika category ya Makeup Artists. Ni furaha kuona Mtanzania ameweza kuonyesha kipaji chake na kuwa wa kwanza hapa nchini Italia.
Abbia Maswi alizaliwa Tanzania na Baadae aliungana na Mama yake nchini Italy ambapo alipata elimu yake tangu chekechea hadi chuo kikuu.
Kwa sasa Abbia anafanyakazi na makampuni mbalimbali katika sekta ya mitindo na sinema