1 0
Read Time:1 Minute, 6 Second

Na Mwandishi wetu WU® MEDIA

Kizazi kipya cha Diaspora Ughaibuni kinavyo itangaza TANZANIA kimataifa

Tatyanna Juma ashinda Miss Elegance mkoa wa Campania Italy 2022

Tatyanna Juma ni Msichana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 18, amezaliwa Tanzania miaka 18 iliyopita. Tatianna aliungana na Mama yake kwenda ughaibuni akiwa Bado hata kuanza chekechea hivyo amepata masomo yake ya awali nchini Italia na sasa Yuko mwaka wa Tano na wa mwisho Diploma yake ya Uongozi Uchumi na masoko.

Tatyanna ni mwanamitindo, alieanza fani hiyo akiwa Bado mdogo zaidi na hivi Karibuni ameshinda nafasi ya kwanza mashindano ya ulimbwende MISS ELEGANCE mkoa wa Campania na Baadae tena ameshiriki mashindano mengine Miss Blumare na kushika nafasi ya pili.

Tatyanna pia amepata kushiriki katika video mbalimbali za muziki.

Mbali na ushiriki wake wote huo lakini pia ni maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii hasa TikTok ambako ana wafuasi wengi.

Alipokuwa akiongea na Mwandishi wa WABONGO UGHAIBUNI MEDIA WU®

Taty alisema “Ninapenda kufanya kazi katika ulimwengu wa burudani kwa ujumla na kufanya mambo mengi mapya, ili kupata uzoefu mpya na kukutana na watu wenye mawazo mazuri na chanya”

Tatyanna katika umri mdogo alishiriki short film akiwa na mama yake iliyoongozwa na director Kader Alassane Alasko “MASIKINI MKWELI”

Short film “MASIKINI MKWELI”
Tatyanna ashika nafasi ya pili
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %