Na Mwandishi wetu WU®
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumeonekana taarifa inayonyesha kitambulisho Cha Taifa Cha Tanzania.

Sintofahamu hiyo imezuka pale ambapo picha na jina linaonyesha mwenye kitambulisho hicho Cha Taifa ana asili ya Asia sambamba na jina ambalo linasomeka katika asili hiyo.
Kufuatia sintofahamu hii ya kitambulisho cha Taifa, Wabongo Ughaibuni Media waliamua kupata maoni kutoka Nyumbani Tanzania, Na majibu au uchambuzi wa taarifa ulikuwa hivi;
Katika kitu kisichopendwa kabisa na Watanzania, hasa serikali ni ubaguzi kwa msingi wa rangi, dini ama kabila.
Tanzania ina aina tatu za uraia;
1.Uraia wa kuzaliwa
2.Uraia wa kurithi
3.Uraia Tajinisi
Aina zote zipo kwa mujibu wa sheria na taratibu. Sheria hizo hazibagui mtu yeyote. Kila anayekidhi vigezo hivyo anaweza kupata uraia. Na anayekiuka anapoteza uraia
“Hicho kitambulisho sidhani kama ni halali”.
Umekisoma namba zake? (“Mdau alimuuliza mwana Habari wa WU®”)
Fungu la kwanza huwa ni mwaka, tarehe na mwezi wa kuzaliwa. Hebu lisome hilo fungu.
Hata hivyo hata kama kingelikuwa ni cha kweli isingekuwa nongwa.
Zamani Waasia wengi(ukiacha wahindi) hawakupenda kuwa raia wa Tanzania ama hawakupenda kupoteza uraia wao wa awali. Hivyo ilikuwa nadra kumkuta mtanzania mweye asili ya bara Asia isipokuwa wahindi.
Tanzania imeendelea sana hivi sasa imeendelea sana. Miundo mbinu ya biashara ni mizuri sana. Kuna fursa za kila namna. Hata wachina wanaona kumbe wanaweza kuupoteza uraia wao ili waupate uraia wa Tanzania.
Kwa sasa hakuna mgeni anayeibeza Tanzania. Thamani ya nchi ipo juu pengine kuliko nchi nyingi za ulaya, Asia na America.
Hivyo wapo wanaoomba uraia tajinisi, na wanaokidhi vigezo wanapewa uraia huo.
Sasa mtanzania asilete nongwa kwa kuwa m- Asia amepewa Uraia wakati yeye kaupoteza uraia wake. Ni hivi; huyo aliyepata utanzania, kaupoteza uraia wake kama ambavyo wewe mtanzania umeupata umarekani baada ya kuupoteza utanzania.








