0 0
Read Time:1 Minute, 11 Second

WU®MEDIA 2024
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ameeleza sababu za mchango wa Watanzania waishio nje ya nchi (diaspora) kuwa mdogo huku akieleza namna “hadhi maalumu” itakavyoongeza mchango wao kwa Taifa.

Makamba amebainisha hayo kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyiofanyika Alhamisi Machi 21, 2024 ambapo amezungumzia masuala tofauti ikiwemo tathmini yake ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.

Pia, ameeleza juu ya utaratibu wa “hadhi maalumu” utakaotolewa kwa raia wa matatifa mengine wenye asili ya Tanzania ambao utapitishwa kwenye mkutano ujao wa Bunge ambapo sheria mbili zitafanyiwa marekebisho; Sheria ya Uhamiaji, ili kuruhusu vibali vipya ambayo haina ukomo, na Sheria ya Ardhi, ili kuruhusu umiliki wa ardhi.

Akizungumza kwenye mahojiano hayo, Makamba amesema diaspora wana mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa kwa maana ya kuleta fedha nchini hadi kufikia dola 700 milioni (Sh1.77 trilioni) kwa mwaka.

Hata hivyo, amesema kiwango hicho ni kidogo ukilinganisha na mataifa mengine kama Nigeria ambayo mwaka jana walichangia dola 25 bilioni na Kenya ambayo diaspora wanachangia dola 4.19 bilioni kwa kipindi hicho.

Makamba amesema kuna changamoto mbili kwa diaspora wa Tanzania kuwa na mchango mdogo ukilinganisha na mataifa mengine; mosi, Watanzania wamechelewa sana kutoka nje, nchi nyingine, watu walianza kutoka tangu miaka ya 1950 lakini Tanzania ilibaki nyuma na akuwa shughuli zao huko nje si zenye kutoa kipato kikubwa.

(Imeandaliwa na @geofrey_j2)

Msikilize MH Waziri

Happy
Happy
50 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
50 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %