


Mwaka 1993 niliondoka kuelekea Sydney Australia ambako niliendelea na sanaa za mapambano chini ya sensei Watanabe nilifuzu kupanda ngazi ya mkanda mweusi (black belt) mwishoni mwa mwaka 1994
Baada ya kushiriki katika michuano mingi nilipata kutambua tofauti kati ya sanaa mbali mbali kiuwezo nikaamua kupanua upeo kisanaa,kwa miaka mingi iliyofuatia nilijifunza style nyingine pia kama phillipino Kali, Arnis de mano, boxing, na kick boxing, Aikido na wrestling pamoja na Brazilian Jiu Jitsu na kushiriki katika mashindano mengi ambapo nilijinyakulia medali nyingi na matuzo tofauti ya ushindi!
Kutokana na ushiriki na uzoefu wa miaka mingi kwa sasa hivi Nimebahatika kuwa na nafasi kama mwalimu mkufunzi wa sanaa mbalimbali hapa Sydney hivyo basi nimekuwa nafundisha wapiganaji wa Karate, boxing , Kickboxing, Mixed martial arts,na kupata mafanikio mengi ya ushindi katika mashindano mbalimbali tofauti ya kimataifa.
Mipango ya baadaye ni kujaribu kusaidiana kupanuana kimawazo na kushirikana kuelekezana kiujuzi na waalimu mbali mbali wa michezo ya sanaa za mapambano nyumbani Tanzania ili kuwapa nafasi vijana ya kukuza uwezo na vipaji vya kimichezo na kuinua viwango kwa ujumla!
watu kama wewe ndio tunaowahitaji katika kuwasaidia wengine nchini na kuwatia motisha .Mola akuzidishie afya na uzima.
Good work Sensei Eddy!!
Sensei Rumadha
sensei Edgar kaliboti namjua sana hapo Zanaki nilikuwa nae 1979 hadi alipoondoka na kila akija bongo lazina afike dojo kwangu kusaidia vijana na pia kuniwashia moto
Kalibot anatisha nimewashana nae moto sana dojo zanaki enzi hizo
muulizeni sensei Pambwe anamkumbukaje katika moto wa kumite
Eddy wacha sio mchezo
Big up Kal we 26 man
Yuko mwingine sensei Rumadha Romi yuko USA hebu mtauteni ntakupa contact zake nae moto
Sensei Pambwe alinisaidia sana kunoa makwanja kwa miaka mingi, nilikuwa naye msitari wa mbele, alikuwa Karateka shujaa mwenye moyo wa kijasiri na alikuwa rafiki yangu aliyenisaidia sana kimazoezi katika fani ya Karate, tulikuwa pamoja na akina Marehemu Seif bin Rashid el hashmy ( Shaft), Hamis Amani Mlyansi, Moses Beston etc…. hawa watu walinisaidia sana kujenga moyo wa kishujaa na ujasiri wa kivita katika fani ya Karate, mapambano tuliyokuwa tunapambana yalikuwa sio mchezo ha ha ha
Huyu sensei Rumadha alikuwa ni mtu mmoja mpole sana lakini mwenye akili sana katika mbinu za mapambano, alikuwa sio mchoyo wa ujuzi na alinisaidia sana kunifundisha mbinu nyingi za karate kiila mara tulipokutana kufanya mazoezi yetu nje ya Dojo mara nyingi juu ya majumba fulani fulani ya ghorofa hapo Kariakoo!
Pia Na masempai wengi na wanadojo wengi ambao sijawataja majina lakini tulifanya mazoezi makali makali pamoja hapo katika hekalu la kujilinda enzi hizo wote kwa ushirikiano wao pale Dojo walikuwa ni nguzo muhimu iliyonisandia sana kujenga usugu na umahii wa kimichezo !