0 0
Read Time:1 Minute, 52 Second

Na mwandishi AbuLuLuFaJM

WATU SITA WAMEKAMATWA, KWENYE MAANDAMANO YA KUPINGA KARANTINI (LOCKDOWN)
• Takwimu za Wagonjwa na Vifo si za Kweli Zinagushiwa.
• Wananchi Wanatiwa Hofu Hisiyo ya Lazima.
• Vifo Vya Sonini Vimeongezeka Maradufu.
• Talaka Zimekuwa Nyingi na Kuwasonolesha Raia.

Cork, Ireland
Polisi (Gardaí) jijini Cork, nchini Ayalend wamewakamata jumla ya watu sita, wanaume watano na mwanamke mmoja, kwa kuhusishwa na maandamano ya kupinga na kuchoshwa na kukarihishwa na amri ya kuwekwa kwenye Karantini.

Maandamano hayo yalifanyika siku ya Jumamosi, tarehe 6 Machi 2021 na yalikusanya waandamaji wasiopungua 500.

Watu hao walikamatwa kwa kukiukwa amri ya kutotembea umbali wa kilomita tano wa mzingo, ili kuepusha maambukizo ya virusi vya Korona.

Polisi walisema kuwa watu hao waliokamatwa waliamini walikuwa wanasafiri kwenda kwenye maandamano ya kupinga uwepo wa karantini, na kwa kufanya hivyo wamekiuka na kwenda kinyume na kanuni za afya zinazozuia harakati zaidi ya kilomita 5 mzingo kutoka kwenye nyumba unayoishi.

Msemaji wa wanaandamaji hao bwana Diarmaid Ó Cadhla, aliwaambia waandamanaji kuwa maandamano yao ni ya amani na wamefuata na kutii sheria za nchi.

Alisema pia kila mtu ana haki ya uhuru wa kujieleza “bila kuingiliwa”, na kila mtu ana haki ya kukusanyika kwa amani.

Wengi wa wale waliohudhuria maandamano hayo hawakuwa wamevaa barakoa.

Wadukuzi wetu wa harakati hizi za kupinga uwepo wa karantini wanatudokezea kwa kusema kuwa, maanadamano haya ni moja ya njia ya kuishinikiza serikali kuondoa vizuizi vyote vinavyohusishwa na Korona na wanawaunga mkono wenzao walioandamana uko mji mkuu wa Ayalend Dublin, ila wanapinga fujo zilizosababishwa na Polisi.

Baadhi ya madai ya waandamaji hao, wanasema kuwa taarifa za ugonjwa wa Korona haswa takwimu zake zimekuzwa sana na hata idadi wagojwa wa korona na idadi ya vifo vilivyotokana na korona si sahihi, taarifa zake zimekuzwa kupita kiasi. Hii imepelekea wengi kuwa na hofu na kusababisha kinga za watu kushuka sana na kupelekea vifo ambavyo vingeweza kuepukika.

Habari zinaendelea kusema kuwa, kwa sababu ya karantini, mahusiano ya wenzi, yameathirika sana, talaka zimeongezeka, utengano wa ndugu, jamaa na marafiki umekuwa mkubwa sana kwa kutishwa na haya maambukizo.

Watu wengi wanakufa kwa magonjwa ya saratani, kifua kikuu, magonjwa ya moyo na maradhi mengine, lakini wote hao wanajumlishwa kuwa wamekufa kutokana na Korona kitu ambacho si kweli na kupelekea watu wengi kupata sononi na hata baadhi ya watu kujiua.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %