Wabongo Ughaibuni WU tunaungana na Watanzania wote popote walipo kuomboleza msiba mkubwa wa taifa letu. Tumezipokea taarifa za msiba kwa mshituko na masikitiko makubwa sana. Nchi yetu ipo kwenye wakati mgumu wa maombolezo ni imani yetu kuwa sote kwa pamoja tutaungana kama Taifa ili tuweze kusimama imara na kuyasimamia yote aliyoyafanya mpendwa wetu Raisi wetu Daktari JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.
Tunatoa salaam za rambirambi kwa serikali zetu zote, Makamu wa raisi Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh . Majaliwa Kassim Majaliwa na Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi.
Kwa kipekee kabisa tunatoa pole kwa Mama JANET MAGUFULI na familia nzima,ndugu jamaa na marafiki wa familia.
Shujaa ameondoka ametuacha tukitembea vifua mbele, MUNGU AMTOA NA MUNGU AMETWAA, TUNAMUOMBA MUNGU KWA HURUMA YAKE AMUWEKE MAHALA PEMA PEPONI. AMIN!
R.I.P JPM