0 0
Read Time:4 Minute, 36 Second

MRADI WA BANDARI YA BAGAMOYO KAMA SEHEMU YA KUVUNA/KUPORA UTAJIRI WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI!

George Michael Uledi.
Kyela, Mbeya!
April 14, 2021.

Saa zingine ni muhimu kujiuliza maswali magumu kwamba Je, Tanzania tuna ndoto ya kuwa Taifa kubwa angalau kwa Afrika tu? Kama jibu ni ndio, je, tunafikaje huko?, nani atatupeleka kwenye ndoto ya kuwa Taifa kubwa angalau katika Bara la Afrika?

Hivi tunaweza kuwa Taifa kubwa kiuchumi kama mpaka leo Taifa lina mawazo ya diplomasia ya kiuchumi ya aina moja ya kuvutia uwekezaji “FDI’s”? Hivi kwa nini hatuwazi kutoka nje ya mipaka yetu na kwenda kuwekeza kama kweli tunataka kuwa Taifa kubwa barani Afrika na baadae duniani?

Utajiri wa leo wa Ulaya kila mtu anajua ulipatikana kupitia uporaji katika mabara mengine na mpaka sasa Ulaya inaendelea kupora utajiri wa Afrika kupitia dhana mpya ya uwekezaji (Ubepari Mamboleo) “Neo-Imperialism”. Nani katwambia Waafrika kwamba tunaweza kuendelea kwa kupitia kutanua uwanja wa Uwekezaji wa nje “FDI”.

Kama kweli tunataka kuwa” The African Superpower” lazima diplomasia yetu ya kiuchumi ianze kuwaza tofauti “two ways flow” kwa maana ya kuvutia wawekezaji lakini pia kupeleka mitaji nje kwenye mataifa dhaifu.

Hili ndio jukumu moja kubwa la idara yetu kuhakikisha tunayatambua mataifa dhaifu kisera na sheria na kutumia fursa hiyo kushauri Taifa kwenda kunyonya uchumi wao na kueneza mila zetu katika Mataifa dhaifu.

Huwa najiuliza, hivi tunashindwaje kama Taifa kutumia madhaifu ya majirani zetu kutanua maslahi yetu?Hivi inakuwaje tunashindwa kwenda kutafuta maslahi yetu Congo ambako mataifa ya Ulaya yamekuwa yakinufaika na utajiri huo sisi tumekaa kimya! Je, ubalozi wetu wa Congo unafanya nini nje ya kulinda maslahi yetu ya kiusalama? Maslahi yetu ya kiuchumi yanapatikanaje?

Viongozi wangu wa CCM wana ndoto ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa kubwa? kama wana ndoto hiyo kweli, tunafikaje? kwa ramani ipi na lini?

CHINA NA MRADI WAO WA KUITAWALA DUNIA KIUCHUMI NA KIUSALAMA.

China Belt & Road Initiative ni mpango mkakati kabambe wa Chama cha Ukomunisti cha China uliobuniwa chini ya gwiji wa siasa Uchumi wa China XI Jinping Rais wa Jamhuri ya watu wa China mwaka 2014.

Nanukuu maneno haya “China’s Belt & Road Initiative forges intertwining economic, political and security ties between Africa and China, advancing Beijing’s geopolitical interests…”.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %