0 0
Read Time:39 Second

16 Aprili 2021

Katika hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemwelezea hayati Magufuli kuwa alijitahidi kupanua huduma za kijamii na kukabiliana na rushwa akisema, “hayati Rais Magufuli alichagiza maendeleo ya miundombinu na viwanda, vitu muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi.” 

Guterres amesema chini ya hayati Magufuli Tanzania ilifikia azma  ya kuwa nchi ya uchumi wa miaka minne kabla ya lengo lililokuwa limewekwa la mwaka 2025. 

Katibu Mkuu pia amegusia elimu akisema kuwa Hayati Magufuli alisaidia kuimarisha mfumo wa elimu na kuongeza viwango vya uandikishaji wa wanafunzi wapya kujiunga na shule za sekondari. 

Halikadhalika serikali yake ya awamu ya tano, iliimarisha usambazaji umeme vijijini ikiwa na lengo la kupanua uwezo wa wananchi kupata umeme nchi nzima.  READ

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %