Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imewahukumu kifungo cha miaka 30 gerezani washtakiwa Damian Jankowsky Krzysztof raia wa Poland na mke wake Eliwaza Raphael Pyuza Mtanzania kwa makosa ya kulima mimea 729 ya bangi na kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi kiasi cha kilogramu 17.2 kinyume cha sheria.
Vilevile, Mahakama hiyo imewahukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani au kulipa faini ya shilingi milioni nne kila mmoja washtakiwa Eliwaza Raphael Pyuza, Hanif Hassanali Kanani raia wa Tanzania mwenye asili ya kihindi na Boniface George Kessy Mtanzania, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya bangi...Read