0 0
Read Time:3 Minute, 42 Second

ASHRAPH. S.KIOBYA
0743405045


Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mnamo saa Kumi kamili tarehe 22/04/2012, Tanzania nzima ilikaa kimya kupisha hotuba ya viwango na yenye kuleta matumaini na mwelekeo wa Serikali anayoiongoza. Hakika kila kona Watanzania walikuwa na kiu ya kutambua nini kitakachojiri hapo Bungeni.
Miongoni mwa nukta muhimu zilizoguswa ni pamoja na yafuatayo.

  1. Pongezi kwa Watangulizi wake katika Uongozi akiwemo Hayati JPM, Dr J. Kikwete na wastaafu wengineo waandamizi.
  2. Kutambua michango ya Wastaafu akiwemo Rais Karume aliyefanya Uteuzi wa Kwanza wa Mh Rais Katika wadhifa wa Uwaziri, Rais Dr. Jakaya Kikwete aliyemteua katika wadhifa wa Uwaziri na katika Bunge la Katiba, lakini pia ametambua mchango wa Hayati Dr. Magufuli kumteua Kama mgombea mwenza kwenye nafasi ya Makamu wa Rais mwanamke aliyeweka historia hiyo (2015-2020) .
  3. Shukrani kwa mhimili wa Bunge kwa kupitisha Azimio la kumpongeza na kukubali pendekezo lake la Makamu wa Rais Dr. Isidory Mpango.
    Serikali ya awamu ya 6itaendelea kudumisha mazuri ya awamu zote zilizopita. Pia itaendelea kufanya mabadiliko ya kisekta katika kukuza uchumi wa nchi yetu.
    MASUALA YA KIPAUMBELE.
    • Kulinda na kudumisha Tunu za nchi yetu (Umoja na Amani)
    • Kuongeza nguvu katika kukuza Uchumi wetu.
  • 6.9% ukuaji wa mwaka
  • 26.6% Ya watanzania maskini kuendelea kuweka nguvu ili kupunguza umaskini wao.
    • Hatua zitakazochukuliwa katika kukuza uwekezaji.
    • Kuondoa baadhi ya vifungu vinavyochelewesha waekzaji.
    • Kudhibiti uzembe na Rushwa
    • Kurudisha Imani kwa wawekezaji
    • Kuwasimamia wafanyabiashara
    • Uwazi wa kutambua miradi ya kimkakati.
    •Kuboresha mazingira mazuri ya kiuwekezaji na ufanyaji biashara.
    • Kuondoa urasimu kwa kiwango kikubwa
    • Kuharakidha vibali vya Leseni kwa wawekezaji.
    •Kupata ardhi kwa wawekezaji ili kuwekeza kiurahisi.
    •Kutoa huduma kwa wawekezaji kwa njia ya mtandao (one stop Centre Service). Kwani Kodi ya forodha inakusanywa 40% na makusanyo ya Kodi za ndani ni 20%
    • Serikali kuendelea kutanua wigo wa ukusanyi Kodi kwa uwanda mpana. Hii itapelekea kuongeza vyanzo vya ukasanyaji wa Kodi.
    • Serikali itapanua uchambuzi wa kinankwa mashirika ya umma ili mashirika hayo yaweze kutoa gawio (Dividends) bila uoga.
    • Serikali kuendelea kutambua mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi nchini mwetu na kuendelea kuzalisha ajira kwa vijana wa kitanzania.
    Serikali itaendelea kusimamia upatikanaji wa vibali vya wafanyakazi wa kigeni bila urasimu .
    SEKTA YA KILIMO
    ~ Serikali kuelekeza nguvu katika upatikanaji wa mbolea, mbegu bora na kuendelea kuajiri wataalam katika taaluma ya KILIMO kwani sekta hiyo unabeba 65% ya watanzania. Serikali inazitambua changamoto katika sekta hiyo Kama uhaba wa mavuno, na tija ndogo ya mazao ya kibiashara.
    • Kuendelea kuwekeza katika kilimo Cha kisasa
    • Kupata mbegu bBora za kilimo
    • Kupata fedha kwa ajili ya mitaji ya KILIMO
    •Kuendelea kuboresha Afya ya udogo.
    • Bima ya KILIMO
    • Kuisimamia kwa karibu Benki ya Kilimo.
    SEKTA YA MIFUGO
    ✓ Kujielekeza katika ufugaji wa kisasa. Pamoja na kuwa na mifugo michache yenye kuwa na uzalishaji mkubwa.
    SEKTA YA MADINI
    Mwaka 2015 kiasi cha 3.4% na 5.2% mwaka 2019 kuchangia kwenye Pato la Taifa. Lakini Sekta hiyo ilichangia $ Bil. 2.7 fedha za kigeni.
    ✓ Serikali kuziba mianya ya utoroshwaji wa madini
    ✓ Kuingia ubia na wawekezajiwakubwa duniani katika kuwekeza kwenye sekta hiyo.
    ✓ Serikali ya awamu ya 6 kuwa na mpango wa kuwaendelezaji wadogo wadogo kwa maslahi ya jamii zetu.
    SEKTA YA MAJI
    ✓ Kufanya mabadiliko makubwa katika Ma Engineer wa Maji mikoani ili kuleta tija na ufanisi wa upatikanaji wa nishati hiyo kwa jamii zetu.
    ✓ Serikali itaendelea kuchimba mabwawa ya maji ya mvua , kuendelea Kulinda vyanzo vya maji, na kutunisha mfuko wa maji ili kuleta ufanisi katika sekta hiyo yenye mahitaji makubwa ndani ya jamii yetu.
    MAMBO YA NJE.
    ✓ Serikali ya awamu ya 6 kuendelea kuajiri watumishi na vitendea kazi katika wizara hiyo.
    ✓ Serikali itafungua Balozi mpya kwenye miji ya kimkakati ili kuimarisha uhusiano mzuri na nchi yetu.
    ✓ Kuangalia kwa ukaribu maslahi ya wafanyakazi na upandishwaji wa madaraja katika sehemu za kazi.
    ✓ Kutoa 10% ya mikopo kwa Halmashauri .
    ✓ Kuimarisha nidhamu kwa wafanyakazi hususani wafanyakazi wa umma.
    MASUALA YA KIDEMOKRASIA.
    √ Kulinda Uhuru wa demokrasia na Uhuru wa watu kwa kufuata misingi ya sheria. Mh. Rais ameahidi kukutana na viongozi wa kisiasa kwa nia ya kuonesha mwelekeo wa Siasa ndani ya nchi yetu.
    WAJASIRIAMALI
    ✓ Kuendelea kuboresha mazingira ya wajasiriamali kwa kuwapatia vitambulisho vyenye alama zinazotambulika. Hii itahusisha Machinga, Mama Lishe na Baba Lishe, Bodaboda n.k
    Hotuba yenye viwango iliyomgusa kila Mtanzania, yenye kuwa na faraja na matamanio wa Serikali ya awamu ya 6 ilidumu kwa takribani dakika 93 iliyojaa onyo Kali kwa watumiaji wa mitandao na wazandi waliojazana uzushi ndani yake. Hotuba ya Mh. Rais imeonesha Dira na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya 6.
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %