0 0
Read Time:3 Minute, 15 Second

MAONI YA ULEDI

George Michael Uledi
Kyela,Mbeya.
May 8,2021.

Kuna kipindi nawaza sana hivi inakuwaje Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa halmashauri umekaa katika kiti chako kwa miaka mitano lakini hauna hata mradi mmoja wa kukuingizia mapato ambao umewahi kuanzisha katika eneo lako.

Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya una kila kila kitu cha kukufanya ufanye makubwa katika kuwaletea watu wako maendeleo kwa maana ya watu na rasilimali nyingi zimekuzunguka katika Mkoa na Wilaya yako!

Pale Simiyu pana kiwanda kikubwa cha chaki ambacho soko lake kubwa lipo Zanzibar na hizi ni juhudi binafsi “initiatives” za RC Antony Mtaka!Mwaka huu niliwahi kushauri kwa kuandika jinsi halmashauri zetu zinavyoweza kutengeneza vyanzo vya mapato na kuepuka utegemezi kutoka Serikali kuu!

Wiki tatu baadae nikaona RAS wa Mkoa wa Simiyu akifungua semina mafunzo kwa Wakurugenzi wa halmashauri zote katika Mkoa wa Simiyu ya jinsi ya kila halmashauri kutengeneza kampuni za kibiashara kwa lengo la kutanua wigo wa mapato hivyo kuweza kufanya makubwa katika maeneo Yao!

Faida za kuwa mbunifu kwa viongozi wetu ni kujaribu kuitua mzigo Serikali kuu hivyo kuchochea maendeleo ya haraka katika ngazi za Mikoa na Wilaya!Faida za kufanya hivyo ni nyingi kwa maendeleo ya haraka kwa Taifa;

1.Tungeweza kuongeza wigo pamoja na ukubwa wa mikopo kwa ya kuwakopesha makundi maalum ya Wakina Mama,vijana na walemavu hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi katika maeneo yetu!

2.Uanzishaji wa makampuni na miradi mingine ingeweza kusaidia utekelezaji wa ilani ya CCM ya Mwaka 2020 mpaka 2025 kwa maana ya kutengeneza ajira kwa vijana hivyo kuisaidia Serikali kuu kutimiza malengo yake.

Tungeweza kutoa ajira kwa vijana wetu hivyo kupunguza namba ya vijana waliopo Mitaani kwa sasa kwa kukosa ajira hivyo kuifanya Serikali kuu kuweza kupumua!

3.Miradi kwa Mfano ya kilimo cha miti ingeweza kuifanya Mikoa au Wilaya kutoa gawio kwa Serikali kuu hivyo kutunisha mfuko mkuu wa Serikali na kumsaidia Mh Rais kuweza kupata mapato zaidi ya kuweza kuhudumia miradi ya kimkakati!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %