JICHO LA ULEDI
George Michael Uledi.n ko
Kyela,Mbeya.
May 23,2021.

Spidi ya maendeleo katika Taifa lolote utegemea uimara wa mambo kadha ya msingi katika Taifa ambayo yanapaswa kufungamanishwa pamoja ili kuweza kupata kitu kinaitwa “common National Direction”.
Sijui kwa kiasi gani kama Taifa tumeweza kuwaza umuhimu wa kufungamanisha dira yetu ya maendeleo ya Taifa dhidi ya watu wetu kwa maana ya Watanzania kwani kwa kushindwa kufanya hivyo tunajirudisha nyuma spidi yetu ya maendeleo kama Taifa.
TUNAWEZAJE KUFUNGAMANISHA WATU DHIDI YA MALENGO YA MUDA MREFU YA TAIFA?
Je,tuna uelewa wa pamoja kama Taifa ya wapi tunataka kwenda kwa kipindi fulani?Inawezekana viongozi wetu wanajua wapi wanataka kutupeleka lakini je,watu wetu wanajua wapi tunataka kwenda kama Taifa?
Mfano,mkulima wa Nchi hii wa kule Kantalamba anajua wapi tunataka kwenda kama Taifa ndani ya miaka ishirini kuanzia sasa?Nani anapaswa kubeba wajibu huu wa kuwafungamanisha Watanzania dhidi ya dira yao ya maendeleo?
Je,Mchimbaji madini mdogo mdogo wa pale Chunya mkoani Mbeya anajua kwa kiasi gani wapi Tanzania inataka kwenda?Walimu je,Askari wetu wa chini kabisa wanajua wapi tunataka kwenda kama Taifa?
Na hapo ndipo kosa letu kubwa kama Taifa linaanzia!Hauwezi ukawa na spidi kubwa maendeleo katika Taifa kama hakuna “common understanding” kwa Watanzania wote wapi tunataka kuipeleka Tanzania ndani ya miaka ishirini.
Lazima malengo ya Taifa yapandikizwe vichwani mwa watu wako ili kuweza kuleta ufanisi na tija katika shughuli za kitaifa.Watanzania wanapaswa kuimba wimbo ambao unaimbwa na viongozi wao kwani bila kufanya hivyo tunajichelewesha wenyewe kama Taifa.









