0 0
Read Time:4 Minute, 32 Second

JICHO LA ULEDI

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
May 20,2021.

JICHO LA ULEDI

Ni kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuwabatiza Watanzania kwa barafu watanzania ambao walishazoea kubatizwa kwa moto!Mama yangu anasema huu ni wakati wa maridhiano na kujenga umoja wa kitaifa kitu ambacho kwangu naunga mkono mia kwa mia.

Swali langu ni la msingi sana kwamba je,Watanzania hawa wanaweza kutumia nia hii njema ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuenenda katika kutii sheria bila shuruti?,Je,watanzania hawa wanaweza kuiona hii kama fursa au baadae watasema Mh Rais Samia ni dhaifu sana?Uoga wangu unaanzia hapo.

Rais Samia Suluhu Hassan amenukuliwa hivi karibuni akiwataka Jeshi la Polisi kukomesha ujambazi unaoanza kuibuka hivi karibuni hasa katika Jiji la Dar es salaam na Mh.Rais akaenda mbali kwa kusema moja ya kigezo kitakachotumika kuteua au kutengua makamanda wa Polisi wa Mikoa kitakuwa uwezo wao wa kudhibiti ujambazi katika maeneo yao.

KWANINI UJAMBAZI UNAANZA KUIBUKA SASA?

Kujibu swali hili niliweza kuongea na kamanda mmoja wa jeshi la polisi na kumuuliza,”kwanini ujambazi unaanza kuibuka sasa?”,jibu lake lilikuwa hivi”..sio tu majambazi,bali watu wengi wanahisi labda kutakuwa na unafuu fulani fulani baada ya kuingia kwa Mama…”

Ni kama Mh.Rais ameshagundua kwamba kuna watu hasa waalifu wanataka kutingisha kiberiti hivyo tamko lake la juzi wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha Polisi aliweka wazi msimamo wake kuhusu kamanda atakayeshindwa kudhibiti ujambazi katika eneo lake la utawala.

Watanzania wanapaswa kutumia vizuri sana huruma hii ya Mama kwani huruma hii ina lengo la kuleta umoja lakini sio kuvunja sheria za Nchi na Serikali ya awamu ya sita kamwe haitosita kuwabatiza kwa moto wale wote watakaovunja sheria za Nchi kwa makusudi.

Watanzania wa kada mbalimbali kwa maana ya Wafanyabiashara,wafanyakazi,Wakulima na wafugaji kamwe wasije wakadhani kwamba Serikali ya awamu ya sita imeenda likizo na eti Rais Samia hawezi kuchukua hatua ngumu na kali kwa wavunja sheria kwa makusudi.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %