0 0
Read Time:3 Minute, 19 Second

Dr Yahya Msangi.

Togo West Africa

Kuna mbunge kanda ya ziwa anaitwa Tabasamu. Katoa hoja kwamba mabwana shamba wenye digrii hawafai wanaogopa umande. Spika kama ambavyo kaanza kujigeuza ndie msemaji bungeni akadakia. Eti mabwana shamba wanaohitajika ni wa chéti. Akadai serikali inafanya makosa kupeleka wenye digrii hâta mashuleni. Eti shule za msingi hazihitaji waalimu wenye digrii Bali wenye vyeti tu. Ili kuonogesha akadai hâta maaskari wanafaa kuwa wa vyeti kwa kuwa Wana nidhamu.
Tanzania ni nchi pekee ina spika na wabunge wanaochukia elimu! Kigezo eti maprofesa wanaharibu.
Majuzi hapa Waziri Ndalichako alisimama bungeni kukemea tabia ya kubeza elimu kwa kuwa inapeleka ujumbe potofu kwa watoto na vijana. Aliuliza: linganisha waliosoma wanaokosea n’a wasiosoma wanaokosea? Kuna msemo “kama unaona elimu ni mbaya basi jaribu ujinga” matokeo nchi imejaa vijana wasio n’a elimu na wanataka ajira, wanatakiwa washindane katoka Soko la ajira n’a wenzao Toka Kenya, Uganda, Rwanda n’a Burundi ambako elimu inatafutwa kwa nguvu zote! Tujisndae vijana wetu kuwa vibarua wa wakenya, warundi, na waganda!

Kwa kuwa kazi yangu ya kwanza maishani ilikuwa wizara ya kilimo nimweleze Spika na Mr Tabasamu haya:

  1. Vyuo vya vyeti vya kilimo waliviua wao kwa kuvinyima mafungu kwenye bajeti. Iko wapi Nyegezi? Chuo Cha Nyegezi walikabidhi majengo kwa kanisa. Wakakihamishia Igurusi Mbeya ambapo kimefia huko. Biko wapi Uyole, UKILIGURU, Nalyendele na kile Cha Agromechanization kule Tanga (jina limenitoka). Maruku ikoje kama sio kiko ICU? Tumbi Tabora kipo? Kilosa kipo? Walioviua sio wao? Hao mabwana na mabibi shamba watashuka toka mbinguni? Viko wapi vyuo vya mabwana shamba wasaidizi vilivyotapakaa nchi nzima mpaka Marangu kwa kina mangi Marealle?
  2. Tatizo la mabwana na mabibi shamba kutiwafikia wakulima sio kiwango Cha elimu au kuongopa umande! Kwanza hawapo! Waliokuwepo waliamua kusepa! Unampeleka Bwana au bibi shamba mmoja wilaya 2 au 3 au kata 10 na humpi usafiri! Atapata kufikia wakulima wote? Unampeleka kijijini bila kumjengea nyumba anaishi kwenye tembe ataacha kurudi mkono ki enjoy ume na internet? Vijijini walivumilia mabwana shamba wa enzi zetu tu. Hawa wa Facebook, Whatsapp na Twitter hawatakaa ng’o! Nilidhani Tabasamu na Spika watajadili haya Badala ya kudai wenye digrii hawafai! Hivi elimu mnaichukia? Mnapeleka waneni shule Ili iweje kama elimu ni jambo baya? Yaani nchi ijae la 7 na Form 4 tu? Au ndio maana sifa mlitoona ya kufaa ni kujua kusoma na kuandika? Kwa taarifa yenu wapo vijana waliotaabika wenyewe kuitafuta elimu wapisheni!
  3. Hivi hâta tungeweza kupeleka maprofesa kufundisha chekechea vijijini si ndio bora? Nani aliwaambia vijijini watoto na wazazi ni wajinga kiasi wanataka waalimu wa UPE? Tutakuwaje uchumi wa kati huku watoto wanafundishwa na waliofeli la 7 au form 4? Uchumi WA kati aina gani huo?

Nilifarijika jibu la waziri husika! Aliona upumbavu huu akaamua awaekeze kidiplomasia !

Wizara jitahidini kufufua vyuo na kuboresha mazingira ya kazi ya mabwana na mabibi shamba wote. wa vyeti, diploma na digrii. Msifanye hui upumbavu wa kuwaondoa wenye digrii kuwabadili na wa chéti. WA chéti asome spare diploma, WA diploma asome apate BSc wa BSc asome apate MSc na wa MSc asome apate PhD. Hoi ndio akili!

Hivi mnataka wa chéti abaki na chéti hadi afe Ili asiambiwe haogopi umande? Akipata Diploma aende Kenya au Botswana?

Msiigeuze nchi kichekesho cha dunia! Mara huku hatutaki barakoa mara hatutaki waliosoma mara tulete matakataka ya Madagascar! Aaargh! Tanzania ni nchi pekee Afrika ujinga umetamalaki! Yaani mpaka tuna Watu wako radhi kupeleka familia jela Kenya huku wanajisifu!

Wizara kile kitengo cha Elimu ya Mkulima kilichokuwa mpaka na gazeti la Mkulima WA kisasa, kipindi RTD na magari ya sinema za kilimo bado kipo? Au maofisa mlikuwa wadogo kipindi hicho hamkukuta?

Spika wewee tafakari kabla hujashauri. Pale Kongwa unategemea Bwana Shamba hâta wa chéti akae? Mna usafiri walau pikipiki? Mna nyumba ya Bwana shamba? Ina umeme na maji? Kuna reliable internet connectivity kama hâta Dar wanakoroma?

Nilidhani ungehitaji mwenye Digrii au hâta professor afundishe kilimo maji (hydroponics), kilimo nyumba (greenhouse agriculture), kilimo hewa (aeroponics)! Aina ya Kilimo Cheney tija, hakitegemei mvua, hakihitaji agrochemicals, n.k. Ndio kwanzaa unataka wa maksai! Kilimo alicho tuacha nacho Chief Kimweri!

Dammit!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %