0 0
Read Time:2 Minute, 4 Second
Katibu mkuu wa umoja wa wazazi Tanzania jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwalimu Erasto Sima

Na.Elisa Shunda,Ngorongoro.
WAKAZI na wananchi jamii ya kimasai wanaoishi katika hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Ngorongoro wameiangukia serikali na kuomba meza ya mazungumzo juu ya taarifa ya serikali kutaka kuwahamisha kutoka kwenye hifadhi hiyo.

Wakizungumza Jana katika nyakati tofauti katika kikao mbele ya Katibu mkuu wa umoja wa wazazi Tanzania jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwalimu Erasto Sima, wakazi hao wamesema walipokea taarifa kutoka mamlaka ya hifadhi Ngorongoro kupitia, Mkurugenzi wake, Manongi kwamba wanatakiwa kuondoka hifadhini humo.

Akichangia katika kikao hicho, Mwenyekiti na Kiongozi wa Lweiganani Ngorongoro, Metui Ole Shaudo, alisema hofu ni tatizo kubwa sana unaweza ukala lakini usijisikie kama umekula kwa sababu ya taarifa ya kuondoshwa kwao katika hifadhi hiyo.

“Kwa zaidi ya miaka 60 wananchi jamii ya kimasai tumekuwa tukiishi katika hifadhi ya Ngorongoro baada ya kuhamishwa na serikali kutoka eneo la Moru Serengeti kupisha hifadhi ya wanyamapori tukaletwa hapa, leo hii tena serikali kupitia mkurugenzi wa hifadhi ya Ngorongoro, Ndugu. Manongi wanataka kutuhamisha tuende wapi” alisema Ole Shaudo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro na Diwani wa Kata ya Enduleni, Emanuel Shangai, alisema awali jamii hiyo ya kimasai baada ya kuletwa Ngorongoro walikuwa wakilisha na kunywesha mifugo yao katika eneo la kreta serikali ikawakataza kwa maana wanawasumbua wanyamapori wa utalii baada ya kuacha eneo hilo kwa sasa limejaa majani wanyama kama swala, pundamilia na wengineo wameacha kula katika eneo hilo na kuwa pori.

Naye Makamu mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya ya Ngorongoro, Foibe Ngangu, aliomba serikali kusaidia jamii hiyo huduma muhimu maji safi na salama, uboreshaji wa miundombinu ya barabara na kuongeza shule za msingi na sekondari ili watoto jamii ya kimasai wapate elimu na vituo vya afya ili wapate huduma bora kama jinsi wakimbizi wanayohudumiwa nchini Tanzania kule mkoani Kigoma.

Akiongea kwa niaba ya wafugaji, Mwenyekiti wa baraza la wafugaji Wilaya hiyo ambae pia ni Diwani wa Kata ya Nainokanoka, Edward Maura, aliomba CCM ielekeze serikali iwekeze katika kutatua changamoto na kero zote zinazowakabili wananchi hao kwa sababu uwepo wao ndani ya hifadhi hiyo ni ulinzi tosha wa wanyamapori na wawatengenezee soko zuri la uuzaji wa mifugo yao.

Akizungumza baada ya kusikiliza maoni yao, Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi, Mwalimu Erasto Sima, aliwaambia wakazi hao kupokea hoja na malalamiko yao amewahahakikishia anachukua changamoto zao na kuziwasilisha katika vikao husika lakini pia akawaahidi kufikisha maombi yao kwa wizara husika na serikali kuu kwa ujumla.

Mwishoo 0719976633

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %