

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 2,2021.
Kuna mambo matatu makubwa yanafanyika leo Tanzania ambayo yanaenda kubadilisha kabisa sura ya uchumi wa Tanzania na “soon” naona tutaanza kumpigia makofi Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ya awamu ya sita.
Huhitaji kuwa Profesa wa Uchumi kuyaona haya yanayoendelea kwamba yanaenda kujenga uchumi imara na fungamanishi katika Taifa ambao unaenda kutengeneza mapato makubwa kwa Serikali,ajira lukuki na kukuza ukwasi katika sekta ya fedha ya ndani hivyo kukuza na kutengeneza fursa zaidi za mikopo kwa wafanyabiashara na wajasiliamali Nchini Tanzania.
Kuna dhana mbili kuu ambazo Serikali yoyote lazima iamue kwenda na moja katika kujenga uchumi wake!Ni kama vile kocha anapoelekea kwenye mechi lazima aamue jambo kubwa moja kati ya mambo makubwa mawili;je aamue timu yake ifunguke au angoje kumsoma mpinzani wake kwanza kwa lengo la kupata ushindi.Dhana hizo kuu mbili ni hizi hapa;
(a)Je,Serikali iamue kujikita katika kuwa mwezeshaji na kuifanya sekta binafsi ifanye kazi.Katika kutekeleza dhana hii Serikali uamua kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya sekta binafsi kufanya kazi na kuna faida kubwa nyingi kuliko hasara ya kutekeleza dhana hii;
1.Serikali inafaidika na fursa za uwekezaji wa ndani na uwekezaji wa nje kwa sababu sekta binafsi inakuwa na imani na mifumo ya kisera na kisheria ya Nchi hivyo kuongeza uzalishaji wa huduma na bidhaa katika Taifa!
2.Ni wakati huu ajira nyingi uweza kutengenezwa na Serikali kupitia sekta binafsi hivyo kuwafanya Wananchi kuweza kuongeza kipato “purchasing power” hivyo kuendesha maisha yao bila kuwa hofu yoyote!Katika wakati huu hautosikia tena vyuma vimekaza kwa sababu mzunguko wa fedha katika uchumi huwa mkubwa na uweza kuwafikia watu wengi zaidi”Money circulation”
3.Ni wakati huu uwezo na wigo wa Serikali kukusanya kodi uongezeka sana hivyo kuiwezesha kuhudumia miradi yake ya kimkakati pamoja na kupeleka huduma bora za jamii kwa watu wake.Ni wakati huu labda Serikali ishindwe yenyewe kukusanya kodi na mapato mengine,kwa kifupi Serikali huwa tajiri zaidi katika kipindi kama hiki.
(b)Je,Serikali ijiingize na kuwa mmoja wa”players” katika kuendesha uchumi wa Taifa kwa maana ya uwepo wa Serikali katika mkono mmoja na uwepo wa sekta binafsi katika upande mwingine.Faida na madhara yake ni haya hapa;
1.Ushiriki wa Serikali katika uchumi kwanza unakuwa na lengo la kulinda rasimali nyeti za Taifa kwa maslahi ya watu wake hivyo Serikali pia uamua kuwekeza na kishiriki katika uchumi pamoja na sekta binafsi kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya Taifa na watu wake.
2.Hasara kubwa ya mfumo huu ni kwamba mara nyingi upunguza imani ya sekta binafsi kwa Serikali hivyo kufanya sekta binafsi”sometimes” kuamua kuamisha mitaji kwenda katika maeneo mengine ya dunia”lost of investors confidence”.Kwa kufanya hivyo uwekezaji wa ndani pamoja na uwekezaji wa nje upungua sana hivyo kuufanya uchumi kushindwa kutengeneza ajira kwa Wananchi wake na hivyo kusababisha mzunguko wa fedha wa ndani kubana”vyuma vimekaza”.
3.Uimara na ukubwa wa sekta binafsi katika Nchi uweza kufungua fursa kwa Wananchi wa kawaida na kuufanya mzunguko wa fedha katika Nchi kuwa mkubwa kutokana na sekta binafsi kuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza ajira nyingi hivyo kuufanya mzunguko wa fedha na huduma kuwa mkubwa “Multiplier effect”.
Kwahiyo ni suala la kocha”kiongozi” kuamua kwenda na mfumo gani kwenye mechi kwa kuangalia kwanza mfumo upi utampa matokeo anayoyataka.








