0 0
Read Time:1 Minute, 39 Second

Na Dr Yahya Msangi

Togo – West Africa

Mheshimiwa nilikusikia ukidai kuwa serikali ikae mbali iache wananchi wajinafasi. Ukidai kuwa wenzetu wanafanya “less governance”. Ukidai umetembelea nchi nyingi ukazitaja ambako uliona less governance.

Kwanza nadhani ulikosea kufananisha governance ulaya na governance Afrika. Hukuwaza kuhusu teknolojia. Kupitia teknolojia serikali za nchi ulizozitaja zinafanya “over governance” ambayo haionekani kwa macho au ndani ya ziara ya muda mfupi. Serikali zao zinajua mpaka chakula unachonunua!

Tanzania na Afrika hatujafika huko. Lazima udhani tuna over governance kwa kuwa governance yetu inapitia kwa watu (human beings) na sio teknolojia kama wenzetu. Chukulia mfano wako wa korosho. Korosho ingekuwa ulaya uuzaji wake usingehusisha jeshi au wabunge. Ungetumika mtandao tu. Je unaweza kutumia mtandao kwa wakulima wetu wa korosho? Hapa nadhani ulisukumwa na chuki dhidi ya mtu. Ni muendelezo wa kauli na vitendo vya usaliti dhidi ya mtu.

Sasa nikujuze kuhusu nchi ambayo kwa bahati mbaya hujaitembelea. Nchi hiyo ni Burkina Faso.

Moja ya tatizo kuu la Burkina Faso (na nchi zote za Francophone) ni “less governance”! Kwao hakunaga sijui cha bwana afya, diwani, serikali ya mtaa n.k.

Burkina Faso ni mfano hai.

Ukiacha mji mkuu wa Ougoudougou serikali haipo kwingine kokote! Nje ya Ougoudougou hakuna wizara, idara wala kiongozi wa serikali. Raia akiwa na shida mfano Ngara atalazimika kwenda Dar Es Salaam! Hâta kusajili uzazi au kifo laxima uende Ougoudougou !
Nje ya Ougoudougou kama hamna mwenzenu serikalini msahau miradi ya maendeleo!

Chanzo kikuu cha mapato serikalini ni dhahabu ambayo imejaa télé Kaskazini Mashariki mwa nchi. Serikali imeacha kampuni 11 za kigeni ichimbe na kuwaondoa wachombaji wadogo waliokuwa wameunda vikampuni 700!

Ni wakazi hao ndio wanaoitwa magaidi! Wamechoka! Huduma za serikali hamna na dhahabu wanachimba wenye héla! Kilimo hakiwezekani ni jangwa!

Badala ya “less governance” hapa suluhu ni “more governance”! Kama ilivyofanya serikali kwenye korosho. Less governance ingeweza kuwaumiza wakulima. Na hakika soko huria (that’s less governance) liliwaumiza wakulima!

Less governance ni soko huria Spika! Same wine in a different bottle!

Niliona mheshimiwa nikupe taarifa. Je umeipokea taarifa ?

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %