0 0
Read Time:4 Minute, 0 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 15,2021.

Kuna kitu kwa muda mrefu kilikuwa kinakosekana katika Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu labda kwa bahati mbaya au labda kwa maelekezo lakini kiweledi naona wazi kulikuwa na pengo la kimawasiliano ambalo labda halikuonekana kutokana na sababu mbalimbali zikiwepo kukosekana kwa “active & vibrant civil societies”vibrant media na “active political parties activities” wakati wa Serikali ya awamu ya tano iliyopita.

Ni wazi kuwa Serikali ya awamu ya sita imekuwa ni muumini wa haki na usawa na kuruhusu Uhuru wa vyombo vya habari,Uhuru wa kufanya siasa na Uhuru wa kujieleza na kukosolewa hivyo kwa sasa kunahitajika uwepo vyombo vya Rais imara na vyenye weledi na uwezo wa kujibu hoja zito zitakazoelekezwa kwa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan kuanzia sasa!

Sina shaka na ninaamini kwa dhati kabisa kuwa,kwa vyovyote vile uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Ndugu yangu Jaffary Haniu ulizingatia sana nyanja hizo nilizozitaja hapo juu!

Wajibu namba moja wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ni kuzitafsiri ajenda kuu ya Rais hasa Rais mpya inayeingia madarakani,kutafsiri maono na dira kuu ya Rais mpya anayeingia madarakani ili Wananchi wa kawaida waweze kuelewa wapi Rais wao anataka kulipeleka Taifa ndani ya kipindi fulani!

Sijui ni kwa kiasi gani wajibu huo umetekelezwa tangu Mh. Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani na kipimo kikuu cha kujua kama wajibu huo umetekelezwa kwa kiwango gani na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ni lazima kifanyike kitu kinaitwa “public opinion survey” ili kuweza kujua je, ni kwa kiasi gani Wananchi wa kawaida wanaelewa ajenda na maono ya Rais wa awamu husika.

Bila Wananchi kuyajua kiundani maono,dira na matamanio ya Rais wao, inakuwa ngumu sana kwa Wananchi hao kumuunga mkono Rais wao kutokana na kutokujua “direction” ya Rais wapi anapotaka twende kama Taifa!Dira na maono ya Rais uweza kusemwa na Rais mwenyewe hasa wakati anahutubia Bunge kwa mara ya kwanza lakini wajibu wa kuhakikisha maono,dira na matamanio ya Rais yanabebwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu kwa kusaidiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali na ikibidi maofisa habari katika kila taasisi,idara na Wizara za JMT.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %