

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 14,2021.
Kwa mujibu wa takwimu za NBS za mwaka 2018 zinasema kuwa,Mkoa wa Kigoma,Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Pwani ndio wazalishaji wakubwa wa zao la mafuta ya mawese Nchini Tanzania,Mkoa wa Kigoma ukizalisha karibia asilimia 61.4,Mkoa wa Mbeya ukizalisha asilimia 35.7 na Mkoa wa Pwani ukizalisha karibia asilimia 0.9 tu hivyo unaweza kuhitimisha kuwa kigoma na Mbeya ndio injini ya uzalishaji wa zao la mafuta ya mawese Nchini Tanzania.
Pamoja na Mikoa hii mitatu kuzalisha mafuta ya mawese lakini bado Tanzania imekuwa ikitegemea kuagiza Nje ya Nchi karibia nusu ya mahitaji yake ya mafuta ya kula Nchini ikiagiza mafuta ya kula karibia asilimia 55.5 kutoka nje ya Nchi pamoja na kuwa na mazingira yote wezeshi ya kuweza kuzalisha mafuta kwa mahitaji ya soko la ndani.
Gazeti la Citizen la Nchini Tanzania la Septemba 18,2018 linaandika kwa Kingereza na hapa nanukuu”….Tz has all it takes to grow and produce enough Palm Oil to meet local demands…….”.
Miaka ya 1980,Serikali ya Malaysia chini ya Waziri Mkuu Mh Mahathar aliona umuhimu wa kulifanya zao la mafuta ya mawese kupitia chikichi kuwa injini ya kuondoa umasikini vijijini”Rural Poverty Reduction Scheme”.
Mwaka 2010,Nchi ya Malaysia iliuza mafuta ya mawese zaidi ya tani 16.7 Milioni yenye dhamani ya dola za kimarekani 15 Bilioni karibia asilimia 9 ya mauzo ya Nje ya Malaysia huku masoko makuu ya mafuta ya Malaysia yakiwa India,EU,Japan,USA,Turkey,Italy na China.
Sekta ya mawese pekee uzalisha ajira zaidi ya 0.8 Milioni katika Nchi ya Malaysia huku ikizalisha ajira karibia 1.7 milioni Nchini Indonesia.Mauzo ya Nje ya mafuta ya mawese kwa Malaysia kwenda Nje yalikuwa 17.368 milioni mwaka 2020.
RAMANI YA KUVUNA FURSA HII KUBWA YA KUKUZA UCHUMI KWA MKOA WA MBEYA TUNAICHORAJE?
Kiwanda cha Bakhresa Group of Company (BGC)kimeihakikishia Serikali kuwa kingeweza kujenga viwanda vikubwa vya mafuta katika Mikoa husika lakini tatizo kubwa wanaloliona ni ukosefu wa malighafi ya mawese katika Mikoa husika hivyo kunahitajika kufanyika kwa mambo haya ili kumvutia uwekezaji katika sekta ya Ki
kilimo vijijini “rural investment”.;
1.Tunapaswa kwa haraka kuanzia sasa kuvutia uwekezaji katika sekta ya kilimo cha chikichi kupitia ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri,Ofisi ya DC na ofisi ya Mbunge hasa katika halmashauri ya Wilaya ya Kyela ambako zao la chikichi ustawi kwa kiasi kikubwa kwa kufanya haya;
(i)Tuanze kuwaanda wakulima wetu kuhusu fursa za kilimo cha mawese kwa kutoa elimu, motisha na fursa za kilimo husika ili kuwaanda wakulima wetu kwa ajili ya kilimo hiki!Lazima tuanze kwa kuleta miche bora ilifanyiwa utafiti na yenye kuleta kilimo chenye tija kwa wakulima kwa maana ya kuzalisha kwa tija!
2 .Pia lazima tuyandae makampuni ya kuwekeza katika sekta ya mafuta ya mawese “Palm Oil Refineries” ili wakulima wabaki kama “collection centres” lakini lazima kuwepo na makampuni makubwa ya kuongeza dhamani ya mafuta ya mawese kwa ajili ya mauzo ya ndani na mauzo ya Nje!
(i) Tunahitaji uwepo wa kiwanda kikubwa cha kusindika mawese katika Mkoa wa Mbeya ambacho kinaweza kujengwa Wilayani Kyela kwa sababu ya ukaribu wa kupata malighafi husika!
Hapa kila Kijiji kinapaswa kuwa na vituo vya kukusanya mafuta ya ghafi ya mawese kupitia “collection centres”hivyo kuongeza ajira kwa vijana vijijini.
FURSA ZINGINE KATIKA KILIMO CHA MAWESE MKOANI MBEYA NI HIZI HAPA!
Kama Mkoa wetu wa Mbeya utaweza kutumia uwepo wa soko na mahitaji makubwa ya mafuta ya kula Nchini hivyo Mkoa husika kuweza kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya. Faida za kutekeleza mradi huu ni hizi hapa.
1.Kilimo cha mawese kinaenda kuondoa umasikini kwa wakazi wa Mkoa Mbeya hasa umasikini wa vijijini “rural poverty”,lakini pia tutaenda kuongeza ajira kwa vijana na wakina mama hivyo kukuza kipato cha kaya na familia!
2.Uwepo wa kilimo cha zao la mafuta Mkoani Mbeya kutaenda kuchochea ujenzi wa barabara na miundombinu ya Maji katika maeneo ya uzalishaji wa kilimo cha mafuta ya mawese!Hakuna kilimo cha mawese bila uwepo wa miundombinu ya barabara katika maeneo yetu.
3.Kilimo cha michikichi kitaenda kusaidia kurekebisha hewa ya ukaa yaani”green house”kupitia uwepo wa miti ya mawese katika maeneo ya kilimo katika Mkoa wa Mbeya.Hii ni fursa ya kuweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya Nchi.
Kuna fursa kubwa na za kimkakati kwa Mkoa wa Mbeya kutekeleza kilimo cha michikichi hasa katika Wilaya za Kyela na maeneo mengine ya kitropiki ambayo zao hili linaweza kustawi katika Mkoa wa Mbeya.
Hivi tunakwama wapi?
Acha Kazi Iendelee!
+255784159968.








