0 0
Read Time:5 Minute, 3 Second

George Michael Uledi
Kyela,Mbeya.
June 13,2021.

Wale wote walikuwa labda wana shaka na msimamo wa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu uimara na msimamo wake katika kulinda rasilimali za Taifa leo watakuwa wamemsikia na wamemwelewa.

Ile propaganda ilikuwa inataka kupandikizwa kwa watanzania kupitia kale kakikundi kapiga ramri chonganishi kamtandaoni kwamba Serikali ya awamu ya sita labda haina ajenda ya kulinda rasilimali za Taifa leo watakuwa wameanza kutafuta ajenda mpya kutaka kuichafua Serikali ya awamu ya sita kwani kwa hotuba yake ya leo kuhusu rasilimali za Nchi hasa madini itakuwa imejibu kila hoja dhaifu za mitandaoni!

“….tuanze kufikilia upya jinsi ya kulinda rasilimali ya madini ya Tanzanite ….madini yetu yanapatikana Tanzania tu lakini leo unaweza kuyapata kwa majirani…..,lazima tufanye re-branding kubwa kuonyesha haya ni madini yetu toka Tanzania…….,Waziri fanyieni kazi hilo haraka…..”.Mh Rais leo amenukuliwa akisema.

Mama Samia,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaona kuna kitu kama Nchi hatujafanya kwenye kulinda rasilimali yetu hasa kwenye madini ya Tanzanite na huo ndio ukweli hasa tukizingatia kwamba Tanzania ndio Nchi pekee duniani yenye kuchimba madini haya ya Tanzanite yaani tuna “competitive advantage” lakini kuna masoko makubwa ya madini haya Nchini Kenya na Nchini India.

Kuonyesha kwamba Mh Rais alikuwa na kitu moyoni kwa muda mrefu kikimsumbua kuhusu jinsi Taifa linavyofanya biashara hii ya madini ya Tanzanite,kauli ya leo wakati anazindua kiwanda kikubwa cha chasafisha dhahabu mjini Mwanza “Gold refinery Plat”.

Akiwa katika moja ya sherehe za kitaifa huko nyuma,Mh Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kunukuliwa akisema”……wakina CDF….ninyi mmejenga ukuta pale Mererani wenzenu wanaiba madini kwa kupitisha chini ya aridhi…….”.

Itoshe kusema kuwa ni wazi Mh.Rais huyu tayari amejipambanua kuwa ni muumini na mlinzi namba moja wa rasilimali za Taifa na nadhani ile hoja ya kwamba tunaibiwa kwa kuuza na baadae mnunuzi wa makinikia kusafirisha mchanga nje ya Nchi inakufa kifo cha aibu!Waziri Mkuu Kasim Majaliwa tayari alishatolea ufafanuzi wa suala hilo Bungeni kwamba kampuni yetu ya kizalendo”Twiga Corperation” ndio inahusika moja kwa moja na uuzaji wa mchanga huo na Serikali kupata fedha yake lakini wenye akili wameelewa!

Hauwezi ukawa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye kila siku anajipambanua waziwazi kwa kutetea rasilimali kubwa za Nchi kama madini alafu leo akashindwe kusimamia rasilimali nyepesi kama mchanga au makinikia ya dhahabu!Watanzania lazima tutafute ajenda za maana na sio ajenda nyepesi zenye lengo la kumkwamisha utekelezaji wa maono na dhamira ya Rais!

Uthibitisho wa kwamba hata huo mchanga “makinikia ya dhahabu” unaosemekana kuuzwa kwa makampuni ya kuchimba dhahabu ndio huo umefanya makusanyo wa mapato ya TRA kwa takribani miezi mitatu mfululizo “March,April,May” yaendelee kupaa kwa kasi ya ajabu!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %