
Mwandishi:
Mathayo Samson Kizinga.
0718 932 888.

Hebu tujiulize kauli kwamba wananchi wasipolipa kodi nchi itashindwa kujiendesha, sawa! Kwani nchi kujiendesha inawagharamia kina nani? “Ni wale wale wanaolipa kodi”
Elimu, Afya, Maji, Mlo, Malazi, Umeme, Usafiri na Usafirishaji, Burudani na Mahitaji ya Kisaikolojia nk. Haya ni mahitaji yanayobeba maisha yanayohitaji gharama.Kimsingi haya ndio maisha.
Kwanini wananchi wanalipa Kodi? Ili kuipa serikali uwezo wa kiuchumi kuweka mipango/ mikakati na utekelezaji wa huduma kuwafanya wananchi wapate huduma kwa ubora, wakati muafaka na kwa urahisi.
Lakini kuna mambo mawili makubwa;
Mosi kama huduma hazitolewi kwa ubora, wakati muafaka na kwa gharama kubwa maana yake unatengeneza vizazi na vizalia kufa mapema au kuwa masikini daima!
Mbili ; Kama serikali haioni umuhimu wa kuwahudumia wananchi na badala yake kujihudumia yenyewe na viongozi wanaofaidi keki ya taifa, maana yake nchi inawafanya wananchi wanyonge na waendelee kuwa tegemezi na yenyewe iendelee kuwa tegemezi.
Mfano huu wa pili unaakisi muktadha wa mahusiano ya nchi zinazoendelea na nchi mabeberu mfano Marekani, nchi za Ulaya na Uchina zinavyotusumbua na kutunyonya.
Nchi za ughaibuni hazioni haja ya kutoa ushirika au msaada wenye tijara hivyo hutumia akili kubwa kupitia wazalendo wao kunyonya, kudhoofisha au kudhulumu nchi dhaifu. Chaajabu hakuna Viongozi wanaothubutu kukataa hali hizi kama alivyofanya Hayati Dr John Pombe Magufuli(Pata pumziko la amani mzalendo wa dhati), au Muamar Ghadaffi, kwamba mahusiano ya nchi mbili lazima yawe ya kuheshimiana na ya kukubaliana tijara kwa pande mbili si ya kulazimishana, kukandamizana na kudidimizana.
Mfano katika mikataba ya madini Hayati Rais JPM alifanikiwa sana.
Ndani na nje ya nchi za ughaibuni kuna ujasusi wa kidola na kimataifa ukilenga, kujidhatiti Kiuchumi na kijeshi ili kuwafanya wananchi waishi maisha yasiyo na gharama kubwa, wachume kiurahisi nje wapeleke ndani ya nchi zao .Je, nchi za Afrika zimeandaa uwezo mkubwa wa ujasusi(secret service) wa kiuchumi kwa kutumia wazalendo waliojitolea kufa kwaajili ya wananchi?
Je, nchi zimeandaa matajiri wazalendo kama Bilgate wa Marekani anavyotusumbua na wengine wanaotusumbua kwa maradhi na kutuchuma kupitia kutuuzia teknolojia? Ili sasa matajiri hawa walipe kodi yenye tija, waajiri bila kunyonya, wasaidie serikali wakati wa mdororo wa kiuchumi nk. Ama serikali huuacha matajiri wajihangaishe, waibe na wanyonye kwasababu nao wananyonywa na serikali?
Au nchi za Kiafrika zimeandaa wazalendo wa kwenda kupokea maelekezo ya kuja kutekeleza kwa wananchi? Hii ni kwasababu dhana ya kushika madaraka ya dola ni kupata nafasi ya kunyonya wananchi , kuonea na kujilimbikizia kwa rushwa na ubadhirifu na kupata nafsi ya kukaa na kuhongwa na wabwenyeynye?
Mfano mdogo ni kuhusu nchi inaposhindwa kutengeneza walipa Kodi wadogo Sana, wa kati na mapapa. Badala yake nchi kunyonya wananchi kwa kodi kubwa mara mbili ya kipato, hii na kutengeneza wazazi na vizalia masikini na fukara.
Kazi ya wakuu w mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi ni kuandaa mikakati ya kiuchumi.Lakini inakuaje kama wanashindwa kubuni vyanzo vya mapato ya serikali yenye tija? Vipi Kama serikali inawalipa lakini hawatumii wataalamu wa halmashauri kuzalisha? Mfano katika Kilimo, Ufugaji, Viwanda, kuuza huduma, biashara, kuuza rasilimali nk.
Inakuwaje serikali inapotegemea wafanyakazi tu kulipa kodi kubwa kuliko baki katika mishahara yao?
Mfano . Makato ya bodi ya mikopo 15% pennsheni 10%, PAYE 9% Bima ya afya 3% vyama vya kitaaluma 2% nk. Bado mtumishi anakuwa hana uwezo kuwekeza au wa kujenga(Kodi kubwa ya pango inamhusu) kula vizuri, kuhudumia Elimu, maji, Umeme, afya yake na watoto wake na wategemezi.
Mfanyakazi akimaliza utumishi anakuwa fukara ujanani au uzeeni kwanini? Ni busara kumfanya awe mlipa Kodi wa uhakika. Mfano muda wowote au akiamua kuacha ajira apewe pesa yake ya NSSF bila kujali umri , alazimishwe kimasharti ya kupewa pesa kuwekeza kuwa mlipa Kodi, apewe wataalamu wa kumshauri kiuchumi katika halmashauri ambapo pesa zake ataelekeza kuwekeza nk.
Ukweli ni kwamba tuna watu wenye mishahara mikubwa na hawajawekeza, waliong’ang’ana madarakani na kuhudumiwa tu na serikali kwa muda mrefu Sana huku vijana tukikosa ajira, waliostaafu bila kuwekeza, waliostaafu wakafilisika kwa kuwa hawakusimamiwa na serikali.
Hii sio sababu ya nchi zetu kuwa ombaomba , kujipendekeza na kukubali masharti ya hovyo ya Wachina na Wazungu?
KUHUSU WALIPA KODI
Serikali iandae walipa Kodi wadogo Sana, wa kati na mapapa, miradi ya kuuza kwa wanachi na ughaibuni.Iwarahisishie walipa kodi walipe kwa kiwango kisichotafsiri unyonyaji au udidimizaji wa biashara na maendeleo ya familia zao nk.
Moja Mfano Walipa Kodi wakusanywe na watambuliwe Kama walipa kodi wadogo Sana ambao ni wengi sana, walipe kadiri ya asilimia 5% wa kati 10% , Mapapa 20% ya pato lao kwa siku, mwezi au mwaka.
Mbili mfano huduma za kulipia kodi zitambuliwe kwa wingi Sana bila tamaa ya Kodi kubwa sana. Mfano huduma ndogo Sana, kati na kubwa, za lazima Sana zitolewe Kodi ndogo Sana au bure ikiwezekana, Kama maji, chakula, Malazi Afya na Umeme.Kodi ikizidi kuwa kubwa sana ndivyo utegemezi unavyozidi kuwa mkubwa Sana na ndivyo umasikini unavyokuwa mkubwa sana na hivyo kutengeneza wazazi masikini na vizalia masikini na fukara.








