0 0
Read Time:4 Minute, 11 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 2,2021.

Nimemsikia Mh. Rais wangu na Mama yangu Samia Suluhu Hassan, wiki jana akiongea kwa dhati kabisa kuhusu nia yake ya kuufungua uchumi wa Tanzania ambao unasemwa kuporomoka kutoka asilimia 7+ mpaka asilimia 4+ mpaka mwaka 2021.

Kwa tafsiri rahisi ni kwamba,shughuli za kiuchumi katika uchumi mkubwa zimeporopoka sana hivyo kutishia ukwasi wa watu na mzunguko wa fedha japo unaweza kushangaa kwamba, makusanyo ya Serikali hasa kwenye sekta fulani fulani kama madini yalikuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa!

Nataka tuweke mjadala vizuri hapa ya jinsi gani Tanzania inaweza kufungua uchumi wake kwa haraka na kwa uhakika zaidi kwani suala la kuufungua uchumi linaweza likawa ni ishu moja lakini suala la msingi zaidi ni kuwepo kwa muendelezo wa ukuaji wa uchumi huo “economic growth & sustainability”.

KWANINI UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA HAUNA MWENDELEZO?

Uchumi imara na uchumi unaokuwa haraka, kwa maoni yangu lazima ujengwe katika nguzo kuu tatu;

1.Ujengwe katika dhana ya “inclusive economy” kwa maana ya kwamba lazima uwezo wa watanzania kawaida wenyewe kuwekeza na kuzalisha katika sekta mbalimbali za kiuchumi hasa uzalishaji”economic ownership”.Lazima kuwepo na uzalishaji wa bidhaa na huduma ambazo zinawaletea Watanzania kipato katika maeneo yao mfano,uzalishaji katika Kilimo,biashara na huduma ambao utawaletea ukwasi zaidi katika mifuko yao.

Ukiwa na Taifa ambalo angalau asilimia 50 ya nguvu kazi inategemea ajira za kuajiriwa kwenye sekta za uzalishaji,uchumi wako hauwezi kukuwa kwa haraka na uhakika zaidi hivyo kukosa dhana nzima ya “inclusiveness and economic ownership”.

Taifa ambalo linaweza kunyonya angalau asilimia 70 ya nguvu kazi yake kwenda katika kuanzisha shughuli za uzalishaji katika uchumi na sio katika kutegemea ajira,Taifa hilo uchumi wake ukua kwa haraka zaidi na kwa uhakika zaidi ” economic growth & sustainability”.

Kwahiyo njia pekee ya kufanya uchumi wa Tanzania ukue kwa haraka na kwa uhakika ni kuiwezesha nguvu kazi kuzalisha na sio kuwezesha nguvu kazi kupata ajira za kuajiriwa katika sekta nyingine!Hii ndio njia ya uhakika ya kufungua uchumi imara na uchumi wa uhakika katika Taifa lolote duniani!Hakuna njia nyingine zaidi ya hii!

2.Njia ya pili ya kuweza kufungua uchumi wa Taifa ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na “capital formation” katika Taifa, ambayo mitaji hiyo inaweza kupatikana kwa njia kuu mbili;moja,Watanzania lazima watoke na kampuni zao kwenda kutafuta mitaji nje ya mipaka kupitia masoko mbalimbali ya fedha na kuja kuwekeza Nchini lakini pili lazima biashara za wazawa ziwekeze ndani ya Nchi kutokana na faida wanayopata katika biashara zao.

Uchumi wa Tanzania angalau kwa asilimia 45 kama ungeweza kuendeshwa na Serikali kupitia mashirika yake pamoja ya wazawa kupitia kampuni zao, unakuwa na uhakika wa ukuaji wa Uchumi imara hasa unapowekeza katika sekta za huduma na sekta za uzalishaji viwandani!

3.Tatu ni Lazima tujenge na kuwezesha makampuni yetu ya ndani mengi zaidi yaweze kutoka na kwenda kuwekeza nje ya mipaka yetu!Makampuni haya yaweza kuwa ya ujenzi,biashara,technolojia,madini na sekta zingine na Serikali lazima iwe na hisa zake katika makampuni hayo kwa lengo la kupata gawio na baadae kuwekeza katika masoko ya mitaji!Ni ujinga sana kuamini kuwa Serikali haiwezi kushiriki katika uchumi wake kupitia makampuni na mashirika yake!

Mfano,Tanzania tunaingia kwenye majadiliano na kampuni ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambayo kwa asilimia kubwa hisa zake zinamilikiwa na Serikali ya China hivyo kuifanya Serikali ya Uchina kuweza kufaidika na ukezaji wa nje wa kampuni hiyo!Tukiwa na kampuni kama hizi nje ya mipaka yetu faida yake katika kukuza uchumi ni kubwa na lazima tutatoboa.

Tanzania kama Nchi lazima tuamue kutoka kwa gharama yoyote ile kwa lengo la kutanua shughuli zetu za kiuchumi nje ya Nchi!Kwanini wenzetu hasa wa China na mataifa mengine yanakuja Afrika?je,wanakuja kutembea?je,wanakuja kutalii?!Hapana!Kuna uchawi mkubwa katika kutoka nje ya mipaka na makampuni yako na lazima tuanze kutoka sasa,hakuna namna!

NAOMBA KUFUNGA KIPINDI HIVI!

Uhakika wa ukuaji wa haraka wa uchumi wetu kama Nchi unaweza kupatikana kupitia”FDI’s” kuja ndani lakini uhakika wa ukuaji wa”economic growth & sustainability” ya uchumi wa Taifa hili utategemea sana mambo makubwa matatu niliyoyajadili kwa undani zaidi hapo juu!Hakuna uchawi zaidi ya huo hapo juu!

Tatizo la FDI’s ni kwamba zinaweza kutupa ajira na kodi kwa muda fulani tu lakini sio kwa muda wote kwani mwekezaji kutoka nje anaweza akabadilisha biashara muda wowote na kufunga biashara yake na kwenda kwao.

Na endapo hali hiyo ikatokea uwezo wa uchumi kuhimili misukosuko hiyo uwa mdogo hivyo kuhatarisha ukuaji wa uchumi wako!Uchumi imara sio ule wa kuamisha mitaji kutoka ulaya kuja Tanzania bali uchumi imara ni ule unaojengwa katika mizizi ya ndani”home based grounded”.

Mimi sio mtaalam wa uchumi lakini nataka mchumi yoyote mbobezi aje na apinge hoja zangu kwa hoja nzito zaidi!Haya ni maono ya kuipeleka Tanzania mbele zaidi leo kesho na milele.

Mwandishi ni Kijana wa CCM,Mkufunzi wa zamani VYUO Vikuu vya Saut na Tumaini,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %