0 0
Read Time:3 Minute, 16 Second

Mwandishi .

Mathayo Samson Kizinga .

0718 932888 .

Kuna uwezekano mkubwa baadhi ya watu binafsi hawatafaidika kama mradi huo wa bandari ya Bagamoyo utamilikiwa na serikali? Hii ni tafsiri rahisi kabisa kuipata kwanini haraka?Kwamba Kuna upigaji umelengwa? Hivyo kwa kujua au kutokujua ushawishi na ushauri mpaka ukubalike?

Awali Hayati Rais JPM aliongea hadharani dhamira yake ya kutaka kuendeleza bandari ya Bagamoyo kwa ushirikiano na China.Baada ya kushauriwa na Injinia Kakonko na pia baada ya kugundua upigaji mkubwa wa mabilioni.(bilioni 115) masharti magumu ya Wachina kujimilikisha ardhi yetu kwa karne nzima(miaka 100) alishituka.
…..ni kichaa tu anayeweza kukubali masharti hayo….Hayati Rais JPM.

Hivyo tunaomba kwanza Rais wetu mpendwa Mh.Samia Suluhu Hassan ajiridhishe kizalendo zaidi! Amen!

…. They presented a very convincing presentation….Mh Job Ndugai.(Spika wa Bunge)
Unategemea laghai
akaongea kwa ulimi wa upanga au ulimi wa kumtoa nyoka pangoni?

….. Unajua nyinyi(Wafanyabuashara wakubwa Tanzania) mna survive kwasababu mnatumia brain(akili nyingi)…. Hayati Rais JPM

Sasa nchi haiwezi kupiga hatua Kama hakuna viongozi wanaotumia akili kubwa kutafsiri mikataba au pia nchi haiwezi kupiga hatua kama Kuna walafi kupitia mikataba.

Wachina Wana survive kwasababu wanatumia ujenzi na uwekezaji ili

1.Kuwatafutia ajira wananchi wake nje ya nchi (to settle extra population ) wakati sisi tuna kozi mia kidogo Chuo Kikuu wasomi wapo mtaani wanasubiri kugawana keki ndogo ya taifa, wanaishia kuichukia serikali na kuwa wapinzani wa serikali.

  1. Kujiingizia pato kubwa toka nje ya nchi badala ya kugombania keki ya nchi.Wanatumia wataalamu waliohitimu vyuo vya kati na vyuo vikuu au wafungwa.Wakati sisi tunagombania vya ndani na kufikiria kodi kupitia makato makubwa ya wafanyakazi na kuwabambikiza kodi wafanyabiashara ndivyo vyanzo vya mapato ya serikali.

Hii ndio tofauti ya brain ya mtu mweusi na mweupe.

Marekani Wana mikakati kabambe ya US CENTICOM (1983) USAID, NATO**, *WB* Mpango ambao unawatafutia ajira wazalendo (Patriots) nje ya nchi na kunyonya iwezekanavyo kibiashara kupitia hata kutafuta chokochoko na kupigana vita ili waingize kampuni zao kuijenga nchi walioibomoa wenyewe na kuchuma rasilimali za nchi husika kisha kuweka stock ardhini mwao US. Rejea vita vya ghuba 1991, vita ya BALKANS, Iraq, na Mapinduzi ya nchi za kiarabu Misri, Tunisia, Sudan na Libya kwa Muamar Ghaddafi.

Sisi tunawafanya nini watu wenye brain kubwa? Wivu, undugu, kujuana nk.Nilichojifunza Afrika mpaka watu wa Chama kimoja wanaharibiana vyanzo vya Kiuchumi na kudhoofishana Kiuchumi au wanatumia akili kubwa kudidimiza wengine ili ku survive badala ya kutumia akili kubwa kutafuta fursa. ( 🦀 Crab Mentality)

Hivyo basi wakati serikali za nchi za nje zinaunda makampuni ya serikali sisi hatutaki kuunda miradi na kampuni za serikali ili kutafutia ajira wahitimu wetu wa vyuo vikuu ndani na nje ya nchi, badala yake tunagombania na kupigania mikataba ya watu weupe iingie kutafutia vijana wao ajira na kushamirisha maendeleo ya nchi zao.

Kwanini tusitumie pesa zetu wenyewe? Kwanini haraka?Kwani tusitumie hata miaka 10 ila mradi uwe wetu 💯% . Kama
gharama ni trilioni 23, mbona Stiglers gorge tumeweza kwa trillioni 13 kwa chini ya miaka mitano? Kwanini tuwamilikishe Wachina?

Wachina wananunua ardhi nje ya nchi ili kuleta extra population mfano Zambia, Sri Lanka, Djibouti, nchi mbalimbali Mashariki ya mbali na Tanzania.

Hivyo Rais wetu kipenzi, Mama yetu Mh. Samia Suluhu Hassan tunaomba usiingizwe mkenge na wasaidizi walafi au wanaotumiwa na watu walafi ili tukupe mitano tena au kumi kabisa tena maana unakwenda vizuri sana.

  1. Turejee RICHMOND, IPTL na ESCROW ACCOUNT . 2.Turejee bogus treaty mfano wa chifu Mangungo wa Msovero .

Kisha tujiulize kama taifa historia inatufundisha nini?

UZALENDO wa viongozi wa Afrika hutia mashaka pale penye conflict of interest na maamuzi dhidi ya matakwa ya kiuchumi ya watu weupe.

Tatizo la watu kupiga kelele dhidi ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo si suala lingine zaidi ya historia ya Wachina na historia ya upigaji dili huku vijana wetu wakitembea na kuhangaika na vyeti na upeo ambao hauna thamani baada ya kuhitimu vyuo.

Ni maoni yangu kwa nia njema ya kizalendo.

Mungu mbariki Rais wetu na Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Mungu Ibariki Tanzania !

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %