
Na Dr Yahya Msangi
Togo -West Africa

Ukiwasikiliza wapinzani uchwara n’a wachambuzu uchwara wa Tanzania utadhani jumuia ya kimataifa inaituhumu tanzania kwa uvunjifu haki za binadamu. Na ukiwa kilaza utaamini. Wengi wanalenga utawala wa awamu ya 5 chini ya almarhum JPM.
Ikiwa utatumikia ubongo wako na sio wa akina Lissu, Fatma, Mbowe na wenzao utagundua hili: umoja WA mataifa hauwezi na Katiba (charter) inawakataza kumuzdhilisha kiongozi ambaye utawala wake unatuhumiwa kuvunja haki za binadamu. Katibu Mkuu anazuiwa n’a kanuni kuongoza kikao cha kumbukumbu ya kiongozi mwenye hizo tuhuma. UN ilitenga kikao maalumu kwa kumbukumbu ya JPM (UN memorial session). Kwa kikao kile UN ilidhihirishia jamii ya kilataifa kuwa utawala wa JPM haukuvunja haki za watu kwa kiwango kisichokubalika kimataifa. Hawa wanaodai alivunja ni mawazo yao. Wapo watu waliamini Yesu na Mohammed walikuwa wahalifu. Lakini haikuzuia utume wao!
Nilimsikikiza Lissu KTN akidai ushahidi kuwa utawala wa JPM ulivunja haki ni kuzuiwa Makonda kwenda US! Ni upungufu wa ubongo kiwango cha juu! Makonda alizuiwa n’a nchi moja. Sio jamii ya kimataifa. Na haki iliyodaiwa kaivunja ni kupinga kutambua mashoga n’a ushoga. Hakutuhuliwa kwa kuvunja haji nyingine zaidi ya hii. Watanzania wengi wako radhi kutoenda US kama sharti ni kutambua ushoga. Kwa waafrika ushoga sio haki ni upotofu na uasi dhidi ya mungu.
Tatizo ni kwamba hâta wanaomtetea JPM hawaujui ukweli huu. Hawajibu kwa hoja bali vioja. UN walimuadhimisha JPM. Ndio ushahidi kwa upande wa haki jumuia ya kimataifa haikuwa na shida naye. Period!
Kwa wasiofahamu utaratibu wa nchi au kiongozi wake kuthibitika anavunja haki tega sikio:
Uhakiki hufanywa na Baraza la Haki za Binadamu (UN HUMAN RIGHTS COUNCIL) lenye makao makuu Geneva. Baraza hili hukutana Kila mwaka ambapo watuhumiwa hutakiwa kujieleza. Watuhumiwa hupatikana Baada ya Baraza kupokea lalamiko lenye ushahidi usio na shaka. Likiridhika ushahidi ni mzito litatuma mkaguzi nchi husika. Kuna mtu, vikundi na NGOs ziliwasilisha lalamiko dhidi ya utawala WA JPM. Baada ya Baraza kupitia vielelezo lilibaini havikuwa na ushahidi wa kutosha. Baraza liliwataarifu wahusika na halikujisumbua kutuma mkaguzi Tanzania. Baadhi ya madhaifu kwenye vielelezo vyao ni: 1 Badala ya kuonyesha tatizo ni la watu wengi wao walioonyesha tatizo ni la mtu au kikundi kidogo cha watu. Walijitahidi kuongeza chumvi ili tatizo lionekane kuubwa ndio maana uliwasikia wakidai Kuna viroba na maiti baharini, Wati wanatekwa kwa maelfu, Kuna maelfu ya wafungwa wa kisiasa gerezani n.k. Walidhani Baraza litakubali TAARIFA ambazo hazina ushahidi. Mfano majina ya hao wafungwa maelfu, majina ya maelfu waliotekwa n.k. Ndio Maana Lissu akitamba kuwa dunia inatutazama na kutakuwa na consequences! Aliamini lalamiko lao litakubalika! 2. Lazima balozi na ofisi za UN zilizoko nchi husika zionyeshe kuwa zinakubaliana na lalamiko . Hakuna hâta Mmoja wao aliyetakiwa kutoa “opinion” aliafikiana na lalamiko! 3. Lazima mtoa au watoa lalamiko waaminike. Ikiwa mfano atajijita au watajikiti kusema Uongo au wao Wenyewe kuvunja haki za wenzao au serikali yao watakuwa wananajisi lalamiko lao. Mara kadhaa mlalamikaji mkuu Lissu ameonyesha kuvunja Haki za wengine zikiwemo Haki za Mkuu wa nchi. Amekuwa akimtukana, kumtuhumu bila ushahidi na kumdhalilisha. Yéyé hakujua haya yanampunguzia sifa kwenye Baraza.
Kuanzia tarehe 21 June mpaka tarehe 15 July kikao cha 47 cha Baraza kinaendelea. Tanzania sio miongoni mwa nchi zinazotakiwa kujitetea! Nchi zilizofikishwa “mahakamani” ni Eritrea, Ethiopia, Belarus, China, Colombia na Myanmar.
Kawaida Kuna mafungu 5 ya mashtaka: closed (haki hamna kabisa), oppressed (haki zimeminywa kisawasawa), obstructed (zimekwazwa kiasi ), narrowed (zimefifishwa) na open (ziko huru kutumia na wote). Katika nchi hizo ni Eritrea pekee ina tuhuma ya ku “close” haki. Wengine karibu Wote tuhuma ni “oppressed”. Watanajitetea huku wahanga nao wakieleza hoja zao. Katika hiki kikao sijaona mshiriki Toka Hao wanaharakati uchwara na wachambuzu uchwara wa siasa! Nadhani kwa kuwa tanzania sio mtuhumiwa wamekata tamaa?
Ukweli ndio huu JPM na Tanzania hawana tuhuma kimataifa!

“Kikao kitapaoisha July nitawapa mrejesho.“