

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 5,2021.
Katiba yoyote duniani mara zote ni chombo cha kutengeneza jamii ambayo kama Taifa mmekubaliana kuitengeneza ndani ya muda fulani kisiasa,kiuchumi na kijamii!kama hivyo ndivyo,ni muhimu sana kujua kwa kiasi gani Katiba hii ya sasa imetimiza malengo na dhamira yetu kama Taifa.
Kuna maswali ya msingi ambayo watanzania tunapaswa kuwahoji wanaotaka Katiba mpya kwa sasa na maswali hayo labda yakijibiwa, tunaweza kuona na kupima uhalali wa mawazo hayo kwa Watanzania!
JE,KATIBA YA TANZANIA YA MWAKA 1977 ILIKUWA INALENGA KUJENGA JAMII YA AINA GANI KAMA TAIFA?
1.Hili ni swali la muhimu sana kuwauliza ndugu zetu wa Chadema angalau watueleze kwamba tulipokuwa tunatengeneza Katiba ya sasa mwaka 1977,Je,tulikubaliana kutengeneza jamii ya aina gani kupitia Katiba husika?Tuanzie hapo!
Unapoona mtu kama John Mnyika,Mdude Chadema,John Hence wanatoa povu kwa kudai Katiba mpya bila kutuambia ni kipi tulikubaliana mwaka 1977 tukipate kutokana na Katiba hii ya sasa!Ni wazi kuwa vijana hawa hawawezi kujibu swali hili kwa sababu hawajui misingi iliyotumika katika kutengeneza Katiba ya mwaka 1977!
2.Je,ni kwa kiasi gani au kwa asilimia ngapi yale majukumu tuliyoipa Katiba yetu ya mwaka 1977 tumefanikiwa kuyapata?Je,Katiba yetu haijaweza kujenga Jamii tuliyokuwa tunaitafuta?jamii yenye mshikamano,amani,upendo,utaifa,undugu,umoja!Haya sio mafanikio?Chadema wanapaswa waulizwe maswali haya ya msingi kabisa!
3.Tuwaulize Chadema kwamba kama Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 imefanikiwa kulinda maslahi mapana ya kiuchumi,kitamaduni na baadhi ya kisiasa kwanini leo tunaona Katiba hii ni ya kishetani?Je tunapimaje ubora wa Katiba,ni wakati gani tunasema Katiba iliyopo ni mbaya?
Mtindo wa Viongozi wa Chadema wa kudokoa kakifungu kamoja kamoja ka kwenye Katiba ya sasa kenye mapungufu na kutengeneza hoja dhaifu haupaswi kuungwa mkono!Tunataka mtu aje na hoja ya Katiba “in totality” na kutuambia ni kwa kiasi gani Katiba hii imeshindwa kutimiza malengo ya Taifa katika nyanja zote na sio kisiasa tu kwani Katiba ni zaidi ya maslahi ya kisiasa!Tukatae!
VYOMBO VYETU VYA SIRI VITUSAIDIE KUJUA HATARI ZA MKUMBO WA KATIBA MPYA.
Naiona hatari kubwa mbele kama vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vitaacha mchakato huu wa Katiba mpya utawaliwe na wanasiasa pekee kwani ni makosa makubwa!Vyombo vyetu katika hili havipaswi kupepesa macho wala kukaa pembeni katika kulinda maslahi ya Taifa na sio maslahi ya Chama fulani!Hatari ninayoiona ni hii hapa;
1.Je,society ya kitanzania ipo tayari kiakili”imegraduate” kuweza kutumia positively mazingira yatakayoletwa na Katiba mpya kwa maana ya Uhuru uliopitiliza?Hili ni swali muhimu sana kwa vyombo kujua maana tusije tukawa tunaleta nadharia na mikumbo ya kudai Katiba mpya wakati jamii yetu bado haijawa tayari!
2.Je,wanasiasa wanawakilisha maslahi ya jamii ya Watanzania au wanawakilisha maslahi yao?Ni muhimu vyombo kujibu swali hilo kabla ya kuruhusu mchakato husika!Maslahi ya wanasiasa hayawezi kuwa maslahi ya Watanzania kwa maana ya Wakulima,wafanyakazi,wavuvi na kadhalika!
3.Hatari ya matumizi mabaya ya Uhuru utakaopatikana kutokana na Katiba mpya yanaweza yakawa makubwa zaidi kuliko madhara yanayoletwa na Katiba ya sasa!Vyombo vyangu vinabidi kuangalia mambo haya kwa jicho la kijasusi na sio jicho la kisiasa!
Namaliza kwa kusema, mahitaji ya jamii na Taifa uamuliwa na jamii yenyewe na always mabadiliko hayazuiliki lakini pia mabadiliko hayalazimiswi,tuache muda uonge!
Mwandishi ni Mkufunzi wa zamani vyuo vikuu vya Saut na Tumaini,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na mtia nia Ubunge CCM Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968








