0 0
Read Time:2 Minute, 33 Second

Na H.Mkali

mkali@live.co.uk

Hivi karibuni alisikika Ndugu Jenerali Ulimwengu katika mahojiano na vyombo vya Habari,akitumia nguvu kumkosoa vikali Mh Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na akafika mbali kwa kusisitiza eti Mh Rais haijui nchi na anafanya makosa makubwa.katika mahojiano hayo pia alimtaja Hayati Rais wa awamu ya Tano Dr Magufuli.hii ni sehemu ya kwanza ya kalamu ya Mkali katika kuichambua hoja za Jenerali Ulimwengu”

Rais Mh.Samia Suluhu Hassan

Mahojiano ya Jenerali Ulimwengu”

Kitu ambacho Ndugu Jenerali Ulimwengu anaonekana kukichanganya katika maisha ni umri na siasa; hivi vitu viwili havitegemeani. Si lazima uwe mzee ili kuwa mwanasiasa bora; kuna vijana wengi wamejipambanua katika siasa duniani. Na kuna wazee waliowahi kuzipeleka nchi zao kwenye maangamizi. Historia ya dunia imejaa tele kweli hii.

Kwani Mwalimu Nyerere alipopewa uongozi wa nchi yetu alikuwa na umri gani? Na alikuwa na uzoefu gani wa kuwa Rais? Lakini leo, Mwalimu Nyerere ni mmoja wa viongozi bora katika historia.

Hivyo kuwapuuza wanasiasa kwa ajili ya umri wao tu, kama ndugu Ulimwengu anavyosema ni kuwa na mawazo ya kisiasa finyu.

Magufuli hakuwa dikteta, bali alikuwa ni kiongozo ambaye ni “hands on and results oriented leader.” Kwa sababu hiyo ilikuwa si rahisi kumdanganya.
Na hiyo ndio iliyomwezesha (katika muhula wa miaka mitano na miezi mitano) kupata matokeo makubwa na mazuri katika nyanja nyingi za maisha ya Watanzania kuliko Rais mwingine yoyote tangu uhuru.
Kiongozi akiharibu, alitumbuliwa tena siyo kwa faragha. Na kuna wengi walikuwa wanafanya mambo hovyo wakiamini hayo yatakuwa ni siri.

Kitu kingine kilichomfanya yeye awe ni tofauti na wengine ni uthubutu au ushujaa wa kipekee katika masuala yaliyohatarisha maisha yake. Na yeye mwenyewe amekuwa ni shahidi kwenye hili.

Alipopewa ushauru uchwara, uwe ni kutoka kwa mataifa ya kibeberu au hizo zinazodaiwa ni taasisi za Kimataifa yeye alizipuuza bila kigugumizi tena hadharani.

Mfano wa karibu, ni Marekani ilipotaka kuzuia uchaguzi wa Zanzibar usirudiwe kwa kuzuia msaada wa pesa za Millenium. Magufuli aliwaambia hizo pesa wala hatukuziweka kwenye bajeti yetu. Hatuzihitaji. Ahsanteni.

Ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Ubungo kwenda Kibaha. “International lenders” walikataa kutoa mkopo wa kujengea hiyo barabara. Magufuli akajenga barabara ya njia nane kwa kutumia fedha za ndani.

Mifano ni mingi mno. Sakata la Uviko-19, Magufuli aliamua kutumia njia zetu wenyewe kupambana nalo (internal solution) na matokeo yalikuwa ni Tanzania kuingizwa kwenye uchumi wa kati mataifa yalipokuwa kwenye timbwili la hili gonjwa la uviko-19.

Nchi za kibeberu zinazojiita zilizoendelea chumi zao zilizorota. Chumi za nchi zote za Afrika zilizokumbatia maelekezo ya kibeberu zote nazo zilizorota.

Magufuli alikuwa kiongozi mahiri wa daraja la Kimataufa. Magufuli alikuwa na uwezo wa kuongoza taifa lolote kati ya hayo mataifa yanayojiita yaliyoendelea.

Kujaribu kumfanya Magufuli aonekane hakuwa chochote ni aidha kukufuru au usaliti au upumbavu/ujinga au hayo yote.

Hivyo basi, Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano ws Tanzania, iwapo unafuata nyao za Magufuli, endelea na huo mwendo. Usisikilize watu ambao hawajui wanachokisema.

Kama kuna watu ambao hawajui ulikotokea, hiyo isikusumbue. Taifa linafahamu. Inatosha.

H. MKALI.
13/08/2021
.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %