0 0
Read Time:3 Minute, 44 Second

Na Dr Yahya Msangi

TOGO – WEST AFRICA 🌍

Sasa hivi balozi zote na JMT zinaendesha zoezi la kutafuta maoni ya diaspora. Leo diaspora ya West Africa ilifanya KIKAO châke kilichoongozwa na Balozi Profesa Bana. Ni zoezi muhimu n’a naipongeza serikali kwa kubuni zoezi hili. Ubalozi umeandaa dodoso ambalo litasambazwa wiki hii kwa diaspora ili watoe mawazo.
Lakini binafsi ningependa kutoa ushauri.

  1. Hili dai la dual citizenship (uraia pacha) litizamwe kwa makini. Nilimsikiliza waziri inaelekea ama anajaribu kuridhisha diaspora ama ana maslahi ya diaspora (sina uhakika). Ila mwelekeo ni Wizara kuona uraia pacha ni jambo zuri. Nilimsikiliza diaspora wanaotaka uraia pacha sababu wanazotoa hazina mashiko. Wengi wanadai wamechukua uraia walipo kwa sababu mbalimbali ikiwa za kuoa au kuolewa au kuhamia. Nikiwauliza ukiamua, kuolewa au kuoa na huku Unajua hasara ya kuukana uraia wa nchi ukiyozaliwa kosa la nani? Si umeamua mwenyewe huo uraia mpya ndio wa maana kuliko wa nchi uliyozaliwa? Iweje urudi kutuambia tuutambue huo uraia mpya wakati ulipokuwa ukiitafuta hukutushirikisha? Hivi huwezi kuoa, kuolewa au kuhamia na ukadumu na uraia wa nchi yako? Mbona tuko wengi wenye hayo na tumeamua tufe na uraia wa nchi yetu? Wizara itafakari sana. Taïfa litapata faida gani kwa kutupa uraia pacha? Taïfa litapata hasara gani kwa kutotupa? Tusitake tu kufurahishana! Hivi mmarekani akachukua uraia wa Afghanistan au Iran watamwelewa? Mbona wapo wengi waliothubutu wameona cha moto?
  2. Diaspora Wanadai wapatiwe vitambulisho vyao eti “DIASPORA ID”. Nikiwauliza hawana Passport? Walifikaje huko waliko? Kitambulisho Cha diaspora kina faida ya ziada (added value) kuzidi passport? Kimataifa kitatambulika na nani? Kwa shughuli gani? Nchini ukarudi na hiyo diaspora ID itatumikaje? Kwani serikali ikaweka register ya diaspora balozini na wizarani haitoshi? Mbona diaspora wengi tu hâta kujitambulisha ubalozini hawafanyi? Mimi pendekezo hili naona ni kituko cha Makolokolo.
  3. Diaspora wengi Wanadai serikali iwape kipaumbele Mwenye Fursa za uwekezaji. Nawauliza msingi wake nini? Upewe kipaumbele kwa kigezo uko nje? Yaani muwe wawili wote Mmoja anaishi Namtumbo mwingine London wewe wa London upewe kipaumbele kuliko wa Namtumbo? Ni kosa kuishi Namtumbo? Sasa ikiwa mwekezaji wa Namtumbo ana ofa nzuri kuliko wewe wa London? Aachwe upewe wewe kisa umetokea London? Si tutabomoa msingi muhimu wa taïfa? Si utakuwa ubaguzi? Kinachotakiwa ni kuondoa bureaucracy kwenye kituo cha uwekezaji ili Kila mtanzania anayetaka kuwekeza awekeze bila kuangalia ni wa Rombo, Cape Town, New York au Lomé! Kituo cha uwekezaji kiwezeshe walio Nje ya Dar Es Salaam kuprocess maombi ya kuwekeza kupitia mtandao (online) mtu awe yuko Kibosho au Stockholm.
  4. Diaspora huwasikii sana wakiongelea wao kulipa kodi kama wenzao walioko nchini. Wanadai tu upendeleo! Serikali lazima iweke utaratibu wa diaspora kulipa kodi. Serikali itofautishe “Kodi/tax” na “michango/remittance”. Diaspora anayeipenda nchi yake hadi kudai apendelewe atakiwe atimize wajibu wake wa kulipa kodi. Mwekezaji gani halipi kodi? Mfano ni diaspora wangapi wamejiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini mwao? Tujifunze Izrael! Diaspora wake hawadai upendeleo! Wanashindana kuchangia uchumi wa taïfa lao asili.
  5. Sio diaspora wote wana faida! Wengine na hakika ndio wengi ni hasara tupu! Hasa diaspora wa Tanzania. Umewahi kusikia diaspora wa nchi ya kiafrika wakiukana uraia wa nchi yao? Umewahi kusikia diaspora wakiandaa midahalo ya kuikashifu nchi yao? Umewahi kusikia wakichangishana Ili mmoja aweze kutukana nchi yao? Diaspora sampuli hii umpe upendeleo katoka uwekezaji? Akiwaleta kina Amsterdam akajifanya ni héla yake? Serikali imeweka utaratibu upi kujua hii ni au sio héla ya huyo diaspora? Inasemekana mapinduzi ya kijeshi na machafuko yaliyoshika kasi West Africa miaka ya 60, 70 na 80 kwa kiasi kikubwa yalichangiwa na diaspora. Serikali iweke iandae:
  6. Code of conduct au ethics itakayotoa muongozo kwa diaspora wote. Ifahamike haya ukiyatenda utapoteza sifa ya kutambulika kama diaspora wa Tanzania. Utabaki na uraia (kama hujaukana).
  7. Serikali iweke makundi ya diaspora (diaspora groups). Mfano: diaspora mwekezaji, diaspora mlipa Kodi, diaspora mtuma miamala , diaspora asiye na mchango wowote kiuchumi. Kuna nchi zimewapa nyota kama za mahoteli na nyingine zinatoa GOLD CLASS, DIAMOND CLASS, BRONZE CLASS, PLATINUM CLASS.

Serikali iwe n’a tahadhari usikubali kuenddzhwa kwa mihemko ya baadhi ya diaspora. Wengi hâta uwezo wa kuwekeza hawana mbwembwe nyingiii. Wangekuwa nao ungeshaonekana.

Awamu ya pili Kuna mtu licha ya kushauriana alileta sera ya kulipana kwa “taaluma maalum”! Walioshauri ni mbaya wakaonekana wamepitwa na wakati! Sasa hili pengo kuubwa la mishahara linalowasumbua litokanalo na ule ushabiki!

Waziri Mulamula akisalimiana na Diaspora alipotemmbelea Kenya hivi karibuni

BALOZI MULALAMULA OVER TO YOU!

Chondechonde usiingize nchi chaka bila tahadhari. Najua inapendeza kuuunga mkono dual citizenship lakini “roses come with thorns mama”! and “beware when Greeks come with presents”! Watakwambia “Sasa umefika wakati” kumbe wanataka kutafuna nchi!

IT’S ME!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %