Na Dr Yahya Msangi
Togo West Africa 🌍
Hakuna kitu kibaya na kinachomdhalilisha mwafrika kama mwafrika kutamani wazungu na uzungu! Kudhani bila mzungu au uzungu hatuwezi!
Asili haswaa ya haya yanayojiri kwenye makoloni ya jamaa ni tabia yao ya kupenda sanaaa uzungu!
Harakati za kudai uhuru zilipopamba moto waliotawaliwa na mwingereza walihudhuria mkutano ambao unafahamika kama LANCASTER CONFERENCE iliyotoka na Azimio na ahadi ya mwingereza kutoa uhuru. Kwa makoloni ya Mfaransa mkutano ulikuwa Elysée Palace. Ikulu ya pale Paris. Na balaa lilianzia hàpo!
Wakati kwenye mkataba wa Lancaster tulidai mwingereza afunge virago aende kwaooo!. Pasibaki chochote chenye kuashiria “imperial authority” kwa wenzetu ilikuwa tofauti.
Kwa uzuzu wa viongozi wao na wengi raia kuhusu uzungu kwenye mkataba wao wakaomba pamoja na uhuru lakini chondechonde mfaransa aendelee kuwatambua kama raia wake wenye haki zoote za raia wa Ufaransa! Wakaomba “Assimilation”! Yaani Sawa wewee udai unataka mamlaka ya mumeo yakome laki aendelee kukupa matumizi!
Mfaransa kina Charles De Gaulle wakajibu “haina shida ila na sisi mtukubalie tuwe na hadhi kuliko taïfa lingine lolote kwenye masuala yafuatayo: fedha, biashara, ulinzi na masuala ya kisiasa. Mkikubali mtakuwa France kama kwenu”!!!
Mapumbavu yakakubali! Mfaransa akaandaa mkataba. Baadhi ya vipengele vinaraka woote watumia faranga itakayosimaliwa na serikali ya France. Katika uchimbaji na uuzaji WA mali asili kwanza auziwe Mfaransa kabla hajauziwa mwingine hâta kama huyo mwingine ana bei nzuriI! Baadhi ya mali iloyojengwa na Mfaransa ikiwemo majengo ziendelee kuwa mali ya Mfaransa! Kituko maarufu ni Jengo la bunge pale Abidjan ! Bunge la Côte d’Ivoire kulikuwa linalipa Kodi ufaransa kwa kutumia Jengo! Bagbo alifuta île kodi mburaaaaa!
Mkataba ule pia ukiitaka wenzetu wachangie uchumi wa France! Si mnaenda kutumia huduma kwa nini mtumie bure? Ikawa maraisi wanashindana kutoa mchango makubwa kuliko wenzake! Ukitoa zaidi unapewa ukiranja wa wenzio! Ndiyo maana hâta wakiwa African Union au UN kuna lmoja wao ndiye kiranja wa Wenzie! Kulikuwepo na kina Houpheit , Bongo, n.k. Akishapewa ukiranja utamjua! Na wenzake woote watamsikiliza. Olé wako uende kinyume na kiranja!
Kusema Kweli héla yao ina Nguvu kuliko yetu. Mfano nikituma Léo Hii faranga 500,000 (laki 5) huko jamaaa atakomba 2,095,110! Milioni 2 aisée!
Cha ajabu mfaransa hazingatii vipengele vingi vya ule mkataba! Mfano sasa lazima waombe visa kwenda France! Lakini jamaa wakikiuka hâta kimoja kinanuka!
Tuwasifu kina Nyerere, Kaunda, Jomo na wenzao! Hawakuhusudu uzungu pale Lancaster ! La sivyo hâta sie ingekuwa hivihivi.