0 0
Read Time:1 Minute, 43 Second

Na Dr Yahya Msangi

TOGO West Africa

“Ni Ushauri wa Dr Yahya Msangi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan”

Mama,

Kwa muda mrefu tulikuwa kimya kuwapa nafasi wenye dukuduku wateme nyongo zao. Sasa imetosha. Hâta Waziri Simbachawene kasema sasa basi! Zamu yetu!

  1. Usijipe “uanajeshi”. Epuka kuvaa kijeshi. Huku nje watashangaa mama kuvaa kombati. Utapoteza sifa nzuri uliyojijengea kuwa wewe hupendi vita na yeyote. Hebu fikiria kama dunia ingemuona Magret Thatcher, Indira Gandhi, Hillary Clinton, Angela Merkel, Kamala Harris wamevaa kijeshi? Uanajeshi sio sifa nzuri kwa wamama wanasiasa. Tuachie wanaume sifa hii.
  2. Epuka kuingiza udini kwenye utawala wako. Umeanza vizuri kwa kuiacha salamu ya kidini. Asalaam aleikum na bwana asifiwe au tumsifu Yesu kristo wasalimiane wahusika Kwenye Nyumba Zao au mikusanyiko yao. Baba wa Taifa alikuwa mkatoliki safi mpaka wenyewe wakataka atangazwe “mtakatifu” lakini hakuwahi kutusalimia kidini. Hakuwa mjinga. Aliweka udini mbali na serikali. Na ikawa salama yetu. Endelea kutusalimia kwa Jina la jamhuri.
  3. Weka ukabila mbali na serikali. Tumia kiswahili popote na muda wote. Kiswahili ndiyo gundi ya taïfa letu. Ukitaka gundi hii iyeyuke ukifika kwenu ongea kwa kikabila chenu. Kuna watu wanadhani huna kabila. Waache wadhani hivyo. Endelea kutumia lugha ya taïfa unapoongea na taïfa.
  4. Tafakari kwa kina ushauri. Nasema hivi maana binafsi naona ushauri usio na nia njema. Mfano: mkakati unaoendelea kuhusu diaspora na uraia pacha. Tulio diaspora tunaona ni kina nani wako nyuma ya huu mkakati. Ni nani kapewa jukumu la kuufanikisha. Sasa hivi Kuna vuta nikuvute huku Nje kuhusu nafasi ya uongozi chama cha diaspora. Waliomaliza muda wao wamegoma kuondoka na wanaotaka uongozi wanaendesha mapinduzi (coupe d’état). Kuna wanaofadhili chama hiki kwa malengo yao. Mama tusipokwambia Sisi akwambie nani? Tunajua maoni yamekusanywa na kutumwa. Huenda maoni ya kizalendo yakaondolewa yasikufikie mezani.

Kwa leo nisikuchoshe! Safari njema NY kwa mkutano wa UNGASS. Nenda mama yapo maslahi ya nchi kayasimamie. A head of State is a Head of state. Huheshimiwa kuliko mwakilishi. Husikilizwa kuliko mwakilishi. Wapuuze wanaotaka usisafiri. Hawajitambui barabara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan

Au revoir et bonne voyage!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %