0 0
Read Time:1 Minute, 58 Second

Na H.Mkali

mkali@live.co.uk

Maelezo ya huyu mchumi hayana mabano.

Ni maelezo ya mchumi kwenye mahojiano na media kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania hasa katika kipindi hiki Cha mdororo wa Uchumi Duniani kutokana na janga la UVIKO 19,Na Nini matarajio ya nchi baada ya kupokea misaada ya pesa yenye lengo la kukabiliana na Hali Hiyo ya mdororo wa kiuchumi. Mwandishi amejibu hoja za mchumi kufuatana na uchambuzi wake”

1) Tanzania hatukuwa na matatizo ya kupata mikopo ya “ku-deal” na janga la Uviko-19. Bali tulikataa kuchukuwa mikopo kwa ajili kukabiriana na ugonjwa huu.

Tulisema: Kama Wahisani wa nje wana huruma na sisi wafute baadhi ya madeni wanayotudai ili tupate unafuu ambao utatusaidia kukabiriana na tatizo la huu ugonjwa. Kutuongezea madeni huko siyo kutusaidia bali ni kutudidimiza. Huo ulikuwa ni msimamo sahihi na wa kuzalendo wakati huo, na ni msimamo sahihi leo na kesho. Kubadili msimamo huo ni kuteleza kwa kiwango kikubwa.

Mtelezo mwingine mkubwa ni kutekeleza mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa kutumia fedha za mkopo kutoka nje. Ili kulinda uhuru na usalama wa nchi yetu, mradi huu utekelezwe kwa kutumia fedha za ndani, fedha zetu wenyewe.

a) Kwa masharti yanayofahamika kutekeleza mradi huu kwa mkopo ni kuuza uhuru wa nchi yetu; na huko ni kusaliti vizazi vilivyipo na vijavyo.

b) Haraka ya kulazimika kuchukuwa mkopo kwa ajili ya mradi huu haipo kabisa kiuchumi na kisiasa.

c) Serikali yetu ilitangaza kuwa majadiliano na Kampuni ya China kuhusu ufufuaji wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo yamefufuliwa.

  • Lakini matokeo ya hayo majadiliano Watanzania hawakutangaziwa.
  • Sasa matangazo yanatolewa kirejareja na “Wachumi’ kuwa ujenzi upo mbioni.
    -Je, huu ujenzi utaanza kwa masharti yepi? Yale yale ya kuuza nchi yetu? Na kama siyo yaleyale kwa nini wahusika wanaleta usiri usiokuwa na maana? Kwa nini wanakuwa na kigugumizi cha kuwatangazia wenye nchi (ambao ni Watanzania wote) hayo masharti mapya ni yepi.

Tahadhari: Uhuru wa nchi yoyote ambayo kweli ni huru, huwa kwa kawaida ni Mali ya Taifa. Siyo mali ya Serikali, siyo mali Bunge na wala siyo mali ya Mahakama Kuu. Uhuru ni mali ya Taifa, yaani mali ya Wananchi wote kwenye nchi husika.

Hivyo, basi Rais, Spika au Jaji Mkuu hawana mamlaka ya kupitisha sheria ambayo hatima yake ni kuuza nchi au sehemu ya nchi. Kufanya hivyo ni kitendi cha kisaliti.

mkali@live.co.uk.
18/09/2021.

Video ya Mahojiano

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %