0 0
Read Time:4 Minute, 6 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Septemba 16,2021.

Kuna wakati fulani niliwahi kufundishwa kitu fulani nikiwa sehemu fulani kwenye kozi ya uongozi”military leadership” kwamba wajibu wa mfuasi ni kumlinda kamanda wako dhidi ya “mashambulizi” ya kimwilini,kimdomo na kimaandishi na kuhakikisha kuwa Kamanda anakuwa yupo salama!

Katika mazingira ya uongozi wa kisiasa bado “practice” na wajibu wa kuilinda mamlaka ya uteuzi unabaki pale pale!Mamlaka ya uteuzi lazima ilindwe na wateule wake kwa gharama yoyote ili kuhakikisha inakuwa salama dhidi ya “mashambulizi” ya mtu yoyote yule! “adui”.

Wajibu huu wa kisiasa kwa wateule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ni wazi kuwa haujaandikwa popote na wala sio wajibu wa kikatiba ndani ya CCM na wala mahali popote.Jeshini Kamanda ulindwa kwa gharama yoyote na wafuasi wake na wafuasi hao watahakikisha kuwa lengo la Kamanda wao “commander’s intent” linatimia kwa gharama yoyote ile!

Kwa maoni yangu,bahati mbaya naona wateule wengi wa Mh.Rais ni wazi kuwa wameshindwa kutimiza jukumu lao la kisiasa kwa kushindwa “kumlinda” Kamanda Mkuu wao ambaye ndiye mamlaka yao ya uteuziMawazo,maono na dira ya Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima
yalindwe,yatetewe,yanadiwe na yasambazwe na wafuasi wake ikibidi ndani na nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!Bado Sijaona bado juhudi za makusudi za kusemea maono mazuri ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan kama ilivyokuwa Serikali ya awamu ya tano ambapo baadhi ya vijana wa CCM na wateule wa Mh Rais waliamua kulibeba jukumu la “kimlinda” Mh Rais waziwazi.

Hivi inakuwaje Mh Rais mwenye wateule katika ngazi mbalimbali kama Wilaya,Mikoa,Wizara hakakosa watu wa kumsemea mitandaoni?Je,wana CCM hatuna cha kusema au hawataki kusema?kwanini Serikali ya awamu ya tano wateule wengi wa Mh.Rais walijitoa waziwazi kumtetea na kuisemea Serikali yake?Hawa wateule wa sasa nini kimewakumba?,yupo wapi Ally Happi yule wa Iringa?,yupo wapi Kibajaj?,yapo wapi makundi ya vijana ya CCM,wapo wapi wote hawa?

UKIMYA WETU HUU NI WA MAKUSUDI AU NI KUTOKUJUA WAJIBU WETU?

Kada wa CCM popote alipo anapaswa kuwajibika kwa chama lakini pia anapaswa kuwajibika kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!Wajibu wetu wa kusema,kutetea na kujibu mapigo yanayoelekezwa kwa chama pamoja na Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa hauna mbadala na wala sio wa kuonea aya!Ni wajibu wa kufa na kupona!

1.Pamoja na nia njema ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwataka wanawake kuchangamkia fursa za uongozi ifikapo mwaka 2025 kauli hiyo imetafsiri kinyume na maadui zetu kiasi kwamba kuzusha mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii!

Ni wazi kwamba mwaka 2025 ndio unaweza ukaweka “heshima” kwa wanawake wa kitanzania pale watapoamua kumpigia kura Mgombea mwanamke na kumwezesha kushinda kiti cha urais wa Jamhuri.

Lazima tukubali kuwa baada ya miaka zaidi ya 50 tokea Uhuru wanawake wa Tanzania wangetamani kuona kwamba ndoto ya muda mrefu ya kutafuta usawa wa kijinsia pamoja na mambo mengine inatimia!Je,kuna tatizo kwa Rais wa Nchi “mwanamama” kulipigia debe hilo?Kama sio yeye nani atapiga debe?

Je,Jumuiya wa wanawake wa CCM wapo wapi kuunga mkono kauli hii?,je,Mawaziri wanawake wapo wapi?,madc wakina Mama wapo wapi?,maras,Maded ,madas wapo wapi?
Hivi wote hawa wangeamua kuvamia mitandao ya kijamii hoja ya Mama inakosaje ushawishi?tumke usingizini!

2.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miezi miwili iliyopita, ameweza kutoa milioni 500 kila wilaya kwa mamlaka ya Tarura ili kuweza kurekebisha barabara katika wilaya zote za Tanzania!Je,wakuu wetu wa Mikoa,Wilaya,Wizara wanatumiaje mitandao ya kijamii kutangaza kazi hizo za Mh Rais?,Je,idara yangu ya Habari Maelezo ni lini iliwaza kuendesha semina kwa wakuu wa Wilaya,Mikoa na Wizara kuwafundisha jinsi ya “kuset” ajenda za Serikali na kuzishambulia kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwapa watanzania taarifa?

3.Ni lini Wizara ya Habari imetumia sekta ya utamaduni,Sanaa na michezo kuweza kutangaza shughuli za Serikali ya CCM na Rais wake kuhusu nini inafanya?,Kwanini “Royal Tour”moja kati ya mradi mkubwa kuwahi kutokea Tanzania haukupewa uzito na wasaani wetu?

Wajibu wa kuisemea Serikali ya awamu ya sita sio wajibu wa idara ya habari-Maelezo
,Sio wa Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Taifa na wala sio wajibu wa Mh Rais pekee yake!Kila mteule wa Rais lazima atumike kama kipaza sauti cha Serikali ya awamu ya sita na Rais wake kwa lengo la kusukuma mbele maendeleo ya Taifa!

UKIMYA huu wa wateule wa Mh Rais unatupa tabu vijana wa CCM kujua je,wateule hawa wanafanya haya kwa makusudi au ni kwamba hawajui wajibu wao kwa mamlaka ya Uteuzi!

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu wa Rais wa zamani, Serikali ya Wanafunzi Daruso-IJMC,Ofisa wa zamani, Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani vyuo vikuu vya Saut na Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %