0 0
Read Time:3 Minute, 51 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Septemba 22,2021.

Biashara ya umachinga katika Afrika inapaswa kutazamwa kwa jicho kubwa na la kipekee zaidi kuliko tunavyofanya leo na tusidhani kuwa watu hawa wanahitaji maeneo yenye usalama ya kibiashara pekee yake kwani biashara ya umachinga inahitaji kupewa jicho kubwa na utafiti wa kitaalam kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale!

Sababu kubwa ya kuitisha utafiti wa kitalaam na utafiti muda mrefu unaoangalia utofauti wa maeneo kati ya eneo moja na eneo lingine unaendana na ukweli kwamba “umachinga” unatofautiana kati ya sehemu moja na sehemu nyingine kwa tabia za biashara!

Karibia asilimia 60 ya ajira zote duniani zinatoka katika sekta isiyo rasmi huku sekta isiyo rasmi ya Tanzania ikiajiri karibia asilimia 75 ya nguvu kazi ya Taifa.Hii ina maana kuwa “umachinga”kwa maana ya wafanyabiashara wasio na maeneo rasmi ya biashara zao”point of sell” ni sehemu moja wapo ambayo inachangia kutoa ajira za moja kwa moja kwa wakina mama na vijana Nchini Tanzania.Je,tatizo la wamachinga “petty traders” je,ni maeneo au ni zaidi ya kuwa na maeneo rasmi ya biashara?

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan hivi karibuni ametoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kote Nchini kuweza kuwatafutia maeneo rasmi wafanyabiashara hawa na kuwapanga kwa utaratibu mzuri zaidi!kwa kifupi ni wazo la kuungwa mkono na kila muumini wa maendeleo endelevu”Sustainable urban planning & management”.

JE,WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA WANAPASWA KUJUA NINI KABLA YA KUANZA ZOEZI HILI?

1.Lazima Serikali kupitia wakuu wa mikoa na wilaya wawe na fikra pana kuhusu kujua mmachinga ni nani na umachinga ni nini?!Umachinga ni utoaji huduma au uuzaji wa bidhaa kwa kiwango kidogo katika maeneo yasiyo rasmi na kama hivyo ndivyo lazima wasaidizi hawa wa Rais wajue kuwa zoezi lililo mbele yao sio jepesi kiasi hicho!

Kwa mantiki pana ni kwamba zoezi ili linaenda kuwahusisha wauza bidhaa ndogo ndogo,bodaboda,vioski vya kupokea na kuweka fedha,wabrashi viatu,wauza chakula mitaani na katika vituo vya daladala na wengineo!Je,wasaidizi wa Rais wana picha hiyo?

2.Je,Serikali inawaza kuhusu kuwawekea miundo mbinu endelevu ya kuwafanya watu hawa waweze kukua na kuja kuwa walipa kodi wakubwa mbeleni?Mshauri elekezi mmoja wa Uwingereza, Bwana Okon Williams, aliliambia jarida la Financial Street kwamba umachinga unaweza kabisa kuondoa idadi kubwa ya watu masikini katika Nigeria.

Nini Serikali ya awamu ya sita inapaswa kufanya ni pamoja na kuunda chombo maalum kwa ajili ya kusimamia sekta ya umachinga Nchini “regulatory agency”!Zaidi ya asilimia 70 ya vijana wa mitaani katika Tanzania wameweza kujiajiri katika biashara ya “umachinga”katika sekta ya bodaboda,chakula,vioski vya miamala ya simu,wauza chipis na sekta ndogo ndogo zingine!Katika muktadha huo unaachaje sekta kama hii kujiendesha kiholela?

3.Wakuu wetu wa Mikoa na Wilaya wanapaswa kuwa na picha kubwa wakati wa kutenga maeneo ya biashara kwa wamachinga kwa kuangalia mambo muhimu ya nani anauza nini na tumpange eneo gani?”market specialisation”.

Ili kuweza kuwafanya wamachinga waweza “kumaintain” wateja wao lazima tutambue maeneo yao ambayo yanawafanya kila siku waweze kupata riziki zao mfano tungeweza kutenga maeneo maalum katika vyuo Vikuu kwa kundi la wamachinga wanauza bidhaa fulani au kutoa huduma fulani kwa lengo la kutowapotezea wateja wao.

Maeneo kama ya hospitali ambayo pia yanawateja wa aina fulani tungeweza kutenga kaeneo kadogo kwa ajili ya machinga wauzao bidhaa zinazoendana na mahitaji ya hospitali kama matunda,chakula na huduma kama hizo!zoezi hili sio jepesi kama wateule wa Rais watakuwa na picha pana kuhusu shughuli za umachinga.

Tutakuwa tunafanya makosa makubwa kwenda “kuwamwaga” machinga wa kila aina katika “point of sell” moja kwa kudhani wateja wao watawafwata huko!Mfano mzuri ni hapa mkoani Mbeya ambapo katika eneo la Bar ya City Pub kuna wamachinga ambao wanaendesha shughuli zao za kuuza nguo na viatu na kuweza kupata wateja wengi zaidi!

Ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba sekta ya umachinga lazima ipewe dhana pana zaidi kwa lengo la kukuza mitaji na kuwawezesha watu hawa kukua na kuchangia pato la Taifa lakini hii itawezekana kwa kuweka mazingira ya kitaalam,kufanya tafiti maalum kuhusu biashara husika.

Ni muhimu Serikali ikajua mambo yafwatayo kwa sasa;ukubwa wa sekta ya umachinga Nchini,je,inaweza kuchangia zaidi ya sasa?,nini kifanyike kuifanya iweze kuchangia zaidi kodi na je,sekta hii inapaswa kusimamiweje ili kuleta ufanisi zaidi na kuchangia katika pato la Taifa!

Mwandishi ni Kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Daraso-IJMC,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri wa zamani Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %